Mjane wa Aboud Rogo kuzuiliwa wiki moja Mombasa


Rogo
Image captionHakimu wamewataka polisi kuheshimu haki za Bi Rogo
Mjane wa Aboud Rogo kuzuiliwa wiki moja Mombasa
Mahakama moja mjini Mombasa imeamuru mjane wa mhubiri wa Kiislamu Aboud Rogo, Bi Hania Saga Rogo, azuiliwe rumande kwa wiki moja kuwapa nafasi polisi kukamilisha uchunguzi.
Upande wa mashtaka ulitaka mwanamke huyo azuiliwe kwa wiki mbili.
Bi Rogo anachunguzwa kwa makosa yanayohusiana na kukusanya pesa za kuwafaa watu wanaojihusisha na ugaidi, wanamashtaka wamesema.
Polisi wanasema alikuwa anawasiliana na mmoja wa washukiwa waliokamatwa kuhusiana na shambulio kituo cha polisi cha Mombasa Jumapili iliyopita.
Simu yake imechukuliwa na maafisa wa uchunguzi kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Hakimu Emmanuel Mutunga amesema polisi wanaweza kukamilisha uchunguzi wao kwa siku saba.
Aidha, ameagiza kuwa haki za mshukiwa ziheshimiwe.
Mawakili wa Bi Rogo walikuwa wamelalamika kwamba polisi wamemzuia kutembelewa na watu tangu alipokamatwa Jumatano jioni.
Washukiwa
Image captionWanawake watatu wanaotuhumiwa kuhusika katika shambulio hilo la Jumapili
Wameambia mahakama kwamba Bi Rogo ana tatizo la kiafya ambalo linafaa kushughulikiwa.
Mshukiwa atarejeshwa kortini tarehe 23 Septemba.
Sheikh Aboud Rogo, alituhumiwa na vikosi vya usalama vya Kenya na nchi Magharibi kwamba alihusika katika kusaidia watu kujiunga na kundi la al-Shabab nchini Somalia.
Hania Rogo na wakili wake Aboubakar Yusuf kortini
Image captionHania Rogo na wakili wake Aboubakar Yusuf kortini
Aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya kutoka Mombasa kwenda Malindi tarehe 27 Agosti, 2012.
Kuuawa kwake kulisababisha ghasia zilizodumu siku kadha mjini Mombasa. Wakati wa maandamano hayo, guruneti lilirushwa kwenye lori la polisi na kusababisha vifo vya watu wawili.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment