MBONI AWAPIGA MSASA VIONGOZI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA


 Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Mboni Mhita  akiwafunda wajumbe wabaraza kuu la UVCCM mkoa wa Arusha

  Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wajumbe waliouthuria mkutano huo
 mjumbe wa Kamati ya utelelezaji Taifa kutoka Mkoa wa Lindi
Amir Mkalipa akiwaasa wajumbe waliouthuria katika mkutano huo

 wa kwanza kushoto ni katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka pamoja naMakamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Mboni Mhita wakisikiliza baadhi ya mambo yalikuwa yakiongelewa katika kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa CCM mkoa wa ArushaBaadhi ya wajumbe wakifuatilia kikao kwa makini 
Na Woinde Shizza, Arusha
 
viongozi na watendaji wa Jumuiya ya vijana (UVCCM)wametakiwa   kutii kanuni  na kuongoza kwa uaminifu ili kuheshimu taratibu zilizowekwa chini ya  misingi ya nidhamu  maadili na kufuata  miongozo ya jumuiya na Chama Cha Mapinduzi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Mboni Mhita  Mara tu alipowasili  mkoani Arusha  kukutana na  kamati ya utekelezaji ya mkoa na kufungua kikao cha Baraza kuu la UVCCM
Mkoa wa Arusha vilivyofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa hapa
 
Mboni aliwakumbusha viongozi wa UVCCM nchini kupitia  viongozi wa Arusha
huku akisiaitiza  Chama Cha Mapinduzi ni taasisi inayoheshimika kitaifa,
kikanda na kimataifa hivyo kila mwana jumuiya  anapaswa kulinda hadhi ya chama hicho mahali popote
  Alisema CCM si chombo kidogo kama ambavyo baadhi ya watu wanavyokichukulia huku akisema  chama hicho ni kikongwe katika siasa  Barani Afrika,kikapata  heshima   na sifa duniani  kwa sera , muundo na misimamo yake katika kupigania haki na harakati za ukombozi Afrika na  nyingine   duniani. 
"Nasisiitiza hatutakuwa tayari kumkubalia, kumsamehe  au kumfumbia macho mwana jumuiya au kiongozi yeyote ambaye anataka kuipaka matope jumuiya yetu ili itafsirike na kuonekana ni genge la maharamia au waganga njaa kwa uzembe na tamaa binafsi " alieleza Mboni .
 
Alisema mwanajumuiya  au kiongozi ambaye hatafuata kanuni zilizopo na
atakayeshindwa  kuheshimu katiba ya chama, akipindisha miongozo au taratibu tulizowekwa , ajiweke  pembeni  mapema kwasababu ccm hakitapata hasara aidha kwa  kujiengua kwa mwanachama au kwa kuenguliwa.
 
"Jumuiya yetu inayoheshimika, ndiyo tanuru na benki ya viongozi wa kisiasa na utawala; hatuwezi kwenda kinyume na  taratibu tulizojipangia
tukaonekana  kama  kundi la kondoo lisilo mchungaji au halina utaratibu
unaoeleweka" alisisitiza Makamu huyo Mwenyekiti
 
Alisema amelezimika kuja Mkoani Arusha kuwaeleza viongozi na wanachama
kwamba kila mwanachama au mtendaji anahitaji kubadilika na kujiendesha
kinidhamu  kulinda hadhi ya chama na isifikiriwe UVCCM si kijiwe cha
mitafaruku kwa mtu anayetaka kuivuruga jumuiya.
 
Aidha Mboni alisema kinachohitajika ndani ya UVCCM kwa wakati huu ni
kuendeleza  mshikamano, umoja, upendo na nidhamu na anayetaka kuuufanya uhuni kuwa sehemu ya siasa afanye  nje ya jumuiya , bila kuuhamishia  utovu huo  wa nidhamu ndani ya  jumuiya .
 
"Mwanachama au kiongozi ambaye anataka kuendesha jumuiya kwa msingi ya uhuni na uchepe alisema ataielewa  UVCCM , hapa si mahali pa
mazingaombwe  ya kihunihuni . tunahitaji matendo ya  utii wa kanuni na
taratibu  ili kupambana na tishio lolote  la uasi au usaliti.
 
Aliwataka  watendaji waliopewa dhamana za utumishi na utendaji waanze
kufanya kazi za  jumuiya kwa kutazama mipaka na wajibu wa kikanuni  ili
kulinda mali na rasilimali za jumuiya mithili ya mboni za macho yao
 
"fichueni na watendaji wanaotuhujumu na ikiwa mna  ushahidi, watajeni
viongozi  wanaotufisidi, wanaotuhujumu na kukwapua mali za jumuiya.
Msiwapakazie watu kwa majungu, chuki au kutaka kuwakomoa na kuwavunjia
heshima zao kwa maneno ya kutungatunga "alisema Mboni
 
Katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka na mjumbe wa Kamati ya utelelezaji Taifa kutoka Mkoa wa Lindi Amir Mkalipa.
Kwa upande wake katibu mkuu wa UVCCM taifa  Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa UvCCM ina miaka 38 sasa ikiwa na heshima ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania hivyo hivyo ili kuifanya UVCCM kuendelea kuheshimika  wanachama wanatakiwa kuwa na umoja na mshikamano  ndio silaha pekee iliyobakia
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment