Maelfu wafika kufanyiwa uchunguzi wa matibabu Tanzania

Wengi waliwasili alfajiri wakisubiri kufanyiwa uchunguzi
Image captionWengi waliwasili alfajiri wakisubiri kufanyiwa uchunguzi

Maelfu wafika kufanyiwa uchunguzi wa matibabu Tanzania-Ni kufuatia uratibu wa mkuu wa mkoa wa DSM Kuhamasisha wananchi kupima afya zao.

Maelfu ya wenyeji wa mji mkuu wa Tanznia Dar es Salaam wamekuwa wakipanga milolongo tangu alfajiri kuweza kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu leo Jumatatu.
Mpango huo ambao ulianza mwishoni mwa wiki uliendelea kwa siku moja zaidi kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza.
Wengi waliwasili alfajiri wakisubiri kufanyiwa uchunguzi
Image captionWengi waliwasili alfajiri wakisubiri kufanyiwa uchunguzi
Wengi wamemuambia mwandishi wa BBC kuwa hawangeweza kukosa fursa hiyo ya kufanyiwa uchunguzi wa bure wa kimatibabu.
Swali ni je, ni kipi kitafuatia ikiwa watapatikana na matatizo ya kiafya.
Wengi waliwasili alfajiri wakisubiri kufanyiwa uchunguzi
Image captionWengi waliwasili alfajiri wakisubiri kufanyiwa uchunguzi
Hakuna matibabu ya bure nchini Tanzania. Watu wazee wanastahili kupata matibabu ya bure, lakini sera hiyo haijatekelezwa kikamilifu.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment