MA DC VIJANA WAMUKUNA RAIS DK MAGUFULI AFURAHISHWA NA UTENDAJI WA KINA DC ALLY HAPI NA RC MAKONDA.
MAGUFULI AKUNWA NA UTENDAJI WA DC HAPI NA RC MAKONDA

Rais Magufuli akunwa barabara na utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe.Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Hapi alipofanya ziara ya Wilayani Kinondoni asubuhi ya leo.

Katika ziara hiyo Mhe Rais  Magufuli ameahidi kuwajengea nyumba wakazi 644 wa Magomeni Kota ambao waliobomolewa  makazi yao  na serikali ya manispaa tangu mwaka 2012.

Rais Magufuli aliendelea kusema Wananchi hao 644 watakaa kwenye nyumba hizo za ghorofa kwa muda wa miaka mitano bure/bila malipo kisha atawafanyia utaratibu wa kuwauzia ili ziwe chini ya himaya zao.

Mhe Magufuli alihitimisha ziara hiyo kwa kuwafagilia DC Hapi na RC Makonda kwa kusema kuwa ni vijana hodari na wachapakazi wanaomuwakilisha vema pia Mhe. Rais amewaasa wasikatishwe tamaa wasonge mbele, wote wanaowakatisha tamaa ipo siku watawaheshimu tu aidha alimpongeza Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kutekeleza agizo lake kwa wakati
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment