Jumba la kumbukumbu za Wamarekani weusi lafunguliwa US


Jumba la kumbukumbu za Wamarekani weusi lafunguliwa Marekani
Image captionJumba la kumbukumbu za Wamarekani weusi lafunguliwa Marekani
Rais wa Marekani Barrack Obama amefungua rasmi jumba la kumbukumbu za Wamarekani-weusi mjini Washington DC.
Obama amesema kuwa jumba hilo la utamaduni na historia ya Wamarekani weusi litatoa historia ya Marekani ambayo haijatambuliwa na wengi.
Mtindo wa Jumba hilo ulichorwa na raia wa Uingereza David Adjaye.
Huku baadhi ya vitu vilivyopo katika jumba hilo vikionyesha wakati wa utumwa, vyengine vinaonyesha utamaduni wa watu weusi ambao umeingia katika utamaduni wa Marekani.
Wanaharakati wa haki za watu weusi nchini Marekani walipendekeza kujengwa kwa jumba hilo mwaka 1915.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment