Bongo kukubali kura zihesabiwe upya Gabon, mahakama ikiagiza

Ali Bongo
BAADA YA KUPATA KIBANO KIKALI TOKA KWA NGUVU YA 'UMMA' HATIMAYE RAIS ALI BONGO ALAINIKA NA SASA AKUBALI KURA KUHESABIWA UPYA.
Rais wa Gabon, Ali Bongo, amesema yuko tayari kutii uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba iwapo mahakama hiyo itaagiza kura za uchaguzi mkuu uliofanyika wiki mbili zilizopita zihesabiwe upya.
Waangalizi wa kimataifa wamesema kuna kasoro nyingi kwenye matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa, ambayo yalimpa Bw Bongo ushindi mwembamba.
Kwenye mahojiano na kituo cha redio cha Ufaransa, Bw Bongo amesema sheria za nchi zake haziruhusu kura zihesabiwe tena.

Waangalizi wa kimataifa wamesema matokeo yaliyotangazwa si ya kuaminikaImage copyrightAFP
Image captionWaangalizi wa kimataifa wamesema matokeo yaliyotangazwa si ya kuaminika
BAADA YA KUPATA KIBANO KIKALI TOKA KWA NGUVU YA 'UMMA' HATIMAYE RAIS ALI BONGO ALAINIKA NA SASA AKUBALI KURA KUHESABIWA UPYA.
Rais wa Gabon, Ali Bongo, amesema yuko tayari kutii uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba iwapo mahakama hiyo itaagiza kura za uchaguzi mkuu uliofanyika wiki mbili zilizopita zihesabiwe upya.
Waangalizi wa kimataifa wamesema kuna kasoro nyingi kwenye matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa, ambayo yalimpa Bw Bongo ushindi mwembamba.
Kwenye mahojiano na kituo cha redio cha Ufaransa, Bw Bongo amesema sheria za nchi zake haziruhusu kura zihesabiwe tena.
Hata hivyo, alisema atakubali hilo iwapo mahakama itaamua hilo lifanyike.
Mahakama ya kikatiba inatarajiwa kukutana Alhamisi kuangazia kesi ya kupinga matoke ya uchaguzi huo ambayo iliwasilishwa na mgombea wa upinzani, Jean Ping.
Ali BongoImage copyrightAFP
Image captionAli Bongo
Bw Bongo alisema suala kuu kwake kwa sasa ni kurejesha utulivu nchini humo na kuiwezesha Mahakama ya Kikatiba ifanye kazi yake.
Ali Bongo alitangazwa mshindi wa uchaguzi, lakini upinzani ukiongozwa na Jean Ping ulipinga matokeo.
Bw Bongo alipata 49.8% ya kura naye Bw Ping akiwa na 48.2%, tofauti kati yao ikiwa kura 5,594.
Bw Ping alishinda majimbo sita kati ya tisa na ameomba kurudiwa tena kwa shughuli ya hesabu ya kura.
Katika jimbo la Haut-Ogooue, anamotoka Bw Bongo, waliojitokeza kupiga kura walikuwa 99.93% kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na 95% ya kura zilipigiwa rais huyo
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment