VIONGOZI AFRICA WAWAKUMBUTIA WATAWALA WA 'MAISHA' IDRIS DEBY AAPISHWA KWA MUHULA WA TANO


Rais wa Chad, Idriss Deby, anaapishwa leo kuiongoza nchi yake kwa muhula wa tano. Viongozi mbalimbali wa Kiafrika wamewasili nchini humo kushuhudia sherehe za uapishaji, miongoni mwao ni Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Deby mwenye umri wa miaka 64 aliingia madarakani mwaka 1990, alishinda uchaguzi wa urais uliofanyika Aprili mwaka huu kwa mara ya 5.

Serikali ya nchi hiyo ilipiga marufuku maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanywa mwishoni mwa juma, kabla ya shughuli ya upishaji.

Hata hivyo, wapinzani walifanya maandamano yaliyosababisha kifo cha mtu mmoja aliyepigwa risasi na vikosi vya usalama. Wapinzani wanatarajia kufanya maandamano zaidi leo, kwa mujibu wa mtandano wa African News.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment