UVCCM WAMPELEKEA MWENYEKITI WA CHAMA DK MAGUFULI MAJIPU YA KUANZA NAYO KUYATUMBUA, YUMO KATIBU MKUU, MCHUMI NA VIONGOZI WENGINE.


 

 VMMU.80Vol.1/46                             14/08/2016
Karibuni sana katika mkutano wetu muhimu tunaofanya leo tukiwa hapa Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha juu cha Jumuiya yetu yaani Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa.

Tarehe 10 Agost mwaka huu kilianza kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kikafuatia kikao cha  Kamati ya Maadili, kufuatia kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa na baadaye Baraza Kuu la UVCCM Taifa. Jumla ya Agenda tisa (9) zilijadiliwa.

Baraza Kuu limeridhika na taarifa kadhaa kuhusiana na agenda mbali mbali na kupokea taarifa moja nyeti na muhimu kwa Jumuiya. “Ripoti ya uchunguzi wa Shamba la UVCCM Na. 454 MBYLR lenye ekari 210” lililopo Igumbilo Wilaya ya Iringa mjini Mkoani Iringa ambalo limeuzwa kwa Ndugu Suhail Ismail Thakore kinyume na taratpia  pia viwanja hivyo kuuzwa kwa watu mbali mbali na kuwahusisha Viongozi kadhaa wenye dhamana ndani ya Jumuiya yetu.

Baada ya kupata taarifa za uuzaji wa shamba hilo Mali ya UVCCM, kwa Mamlaka iliyonayo Kamati ya Utekelezaji Taifa Ibara 91 (d), ilimwachia Mamlaka Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kuunda na kuteua wajumbe watatu wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kuenda kufanya uchunguzi wa kadhia hiyo.

Nichukue nafasi hii kuishukuru kwa dhati Kamati ya uchunguzi iliyoongozwa na;

Ndugu Mariam Chaurembo    -    Mwenyekiti
Ndg Juma Homela  - Katibu
Ndg AmirMkalipa    Mjumbe
Ndugu Ally Nassor  Mjumbe

Kwa kufanikisha kazi waliyopewa na Jumuiya na hatimaye kuwasilisha ripoti yao ambayo ilibaini mambo kadhaa machafu kinyume na miongozo ya Chama na Jumuiya yetu.

Kikao cha Kamati ya Utekelezaji Mkoa wa Iringa kilichoketi Februari 27, 2015 kilipitisha agenda Namba saba kuhusu shamba la Igumbilo na kukubaliana kuuza ekari 20 hadi 30 kwa Shs. 3,000,000/= kwa eka moja, fedha zitakazopatikana zitumike katika Matumizi mbali mbali kwa ajili ya shamba hilo.

Machi 2, 2015 UVCCM Mkoa wa Iringa ilipokea barua toka kwa Ndugu Suhail Ismail Thakore kuomba kununua shamba hilo ekari 30 eneo la Igumbilo kwa bei ya Shs. 3,000,000/= kwa eka ambapo ni sawa na Shs. 90,000,000/=. Machi 4, 2015 Mkataba kati ya UVCCM Mkoa wa Iringa na mnunuzi ulisainiwa rasmi.

Mnamo April 13,17 na 24 Ndugu Suhail aliweka kiasi cha Shs. 90,000,000/= katika Akauunti ya UVCCM  Mkoa wa Iringa Tawi la CRDB.

Shamba la UVCCM Igumbilo ambalo lilikuwa na ekari 210, ekari 85 zilipimwa na kubaki ekari 125. Ekari 85 zilitoa viwanja 170 kwa ukubwa tofauti ambapo ukubwa wa chini sqm 319 na ukubwa wa juu sqm 32,007 ambapo katika viwanja 170 viwanja 25 vikawa miliki ya Ndugu Suhail ambavyo vimetokana na ekari 30 kufuatia mauziano ya sehemu ya shamba hilo kabla ya kupimwa.

Februari 27, 2015, Kamati ya Utekelezaji Mkoa wa Iringa iliketi na kupitisha ili ipatikane fedha kwa taratibu za upimaji na kuomba Hati iliyopo irejeshwe kwa ajili ya kuwasilishwa Halmashauri ya Mji wa Iringa.

Aidha Machi 9 mwaka 2015 UVCCM Mkoa wa Iringa iliandika barua kwenda Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM kuomba kupatiwa Hati ya UVCCM ya umiliki wa shamba la Igumbilo kutoka Makao Makuu ambapo April mwaka 2015 aliyekuwa Katibu Mkuu Ndugu Sixtus Raphael Mapunda aliandika barua kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na kumpeleka nakala Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ili kuikabidhi Hati ya Shamba la Igumbilo.

Machi 29 mwaka 2015 “Special; Resolution Letter” ilisainiwa kati ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Dk. Emmanuel Nchimbi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM Ndugu Sixtus Mapunda ili kuonesha “deed of surrender of right of occupancy”.

UTARATIBU WA UUZAJI WA MALI ZA JUMUIYA NGAZI YA MKOA

Umoja wa Vijana wa CCM  una taratibu zake za uuzaji wa Mali ngazi za Mkoa. Kamati ya Utekelezaji Mkoa itaketi kwa niaba ya Baraza Kuu la Mkoa kuomba kuuza sehemu walioafikiana katika kikao  na kuomba  ushauri na miongozo vikao vya juu.

Kamati ya Utekelezaji Taifa italichanganua pendekezo na kuona kama kuna umuhimu huo na kupendekeza kwa Baraza la Wadhamini. Baraza la Wadhamini litaangalia na kukubaliana au kukataa na kurudisha majibu hayo kwa Mkoa husika.

Katika kadhia hii kilichofanyika ni Kamati ya Utekelezaji Mkoa wa Iringa walikaa na kupendekeza kuomba wapatiwe  Hati Makao Makuu ratibu za kubadilisha matumizina si uuzaji wa eneo kama walivyokubaliana wao kuuza.

Wakati wakiyafanya hayo hapakuwa na kikao cha Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu wala Baraza la Wadhamini vilivyoketi kwa ajili ya utoaji wa Hati au kubariki uuzaji wa eneo la Igumbilo Mkoani Iringa.

Aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa Ndugu Ali Nyawenga aliandika barua kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa kuhusu ombi la mgawanyo wa viwanja ambapo kuanzia kitalu Na. EE 217 – 242 vitakuwa chini ya umiliki wa Ndugu Suhail likiwa na viwanja 25 vyenye ukubwa tofauti.

Kuanzia Kitalu Nambari EE Namba 161 – 216 viliuzwa kwa wananchi mbali mbali, baadhi ya watumishi wa Chama, Jumuiya na Makao Makuu huku Kamati ya uchunguzi ikapata idadi ndogo ya watu waliouziwa kwa uthibitisho wa Risiti na Mikataba.

Kutokana na mapungufu hayo Baraza Kuu la UVCCM Taifa limeamua yafuatayo:-

Kumsimamisha nafasi zote za uongozi ili kupisha uchunguzi Ndugu Seki Kasuga Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa kutokea Mkoa wa Iringa.

Kumsimamisha nafasi zote za uongozi Ndugu Omar Sleiman Mkuu wa Idara ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha wa UVCCM Taifa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mjini – Zanzibar.

Kumfukuza Kazi Ndugu Ally Nyawenga kwa kuuza viwanja vya UVCCM na kuzigawa fedha alizozikusanya kwa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa UVCCM Taifa.

Katibu Muhtasi Upendo Kinyunyu, kwa makusudi aliamua kupotosha taarifa zote alizotoa kwa kamati ya uchunguzi ili kamati ishindwe kubaini ukweli . Aliweza kufuta taarifa na kuficha nyaraka zote ndani ya kompyuta ili kupoteza ushahidi.  Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa imeiagiza Sekretarieti ya UVCCM Taifa kumfukuza Kazi Ndugu Upendo.

Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa imewairudisha Kazini Makatibu wa UVCCM Wilaya zote za Mkoa wa Iringa waliokuwa wamesimamishwa kwa tuhuma ya kupewa viwanja. Kamati imejiridhisha hawakuwa na hatia.

Ndugu Elisha Mwampashi aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa, ambaye sasa ni Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, amekiuka Kanuni za uuzwaji wa eneo la shamba la Igumbilo akiwa Msimamizi Mkuu wa Kanuni ya UVCCM Mkoa Iringa kwa wakati huo.

Hakutoa ufafanuzi wa wazi juu ya matumizi ya fedha zilizoingizwa kwenye Akiba ya UVCCM Mkoa Iringa, ameratibu uuzwaji na upimaji wa eneo la shamba bila kupata idhini ya vikao vya juu ilihal akijua kuwa kufanya hivyo ni ukiukaji wa Kanuni,  Maadili na Katiba ya CCM.

Amekataa kukabidhi Ofisi kwa wakati baada ya kuteuliwa kuwa Katibu wa wilaya ya Iringa Mjini kwa lengo la kuendelea kujinufaisha na mali za jumuiya, akiuza viwanja baada ya upimaji huku akijua anakiuka kanuni za jumuiya, alipokea fedha taslim kinyume na utaratibu, akitoa risiti za uuzwaji viwanja vya UVCCM hali ya kuwa yeye ni Katibu wa CCM na si Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM.

Baraza Kuu la UVCCM Taifa baada ya kuonekana mapungufu na ukiukwaji wa maadili ya Utumishi, Baraza Kuu limeamua tuhuma zao zifikishwe kwa Katibu Mkuu wa CCM ili naye azifikishe kwenye vikao husika kwa hatua zaidi.

Ndugu Hassan Mtenga Baraza Kuu la UVCCM Taifa limebaini kuwa amekubali kuuzwa sehemu ya eneo la shamba, akiwa mjumbe wa kikao huku akijua kanuni hazikufuatwa, kutosimamia jumuiya na Chama ngazi ya Mkoa kuhusu mali za UVCCM, amekubali kupokea zawadi ya kiwanja Kitalu EE 242 kutoka kwa Ndugu Suhail ambaye ndiye mnunuzi wa sehemu ya shamba hilo, akashindwa kuwalisha taarifa wakati wa uuzaji wa viwanja kwa aliyekuwa Katibu wa UVCCM MkoaIringa Ndugu Nyawenga na pia kushiriki  kupokea fedha za mauzo ya viwanja.

Baraza Kuu la UVCCM Taifa baada ya kupokea Taarifa ya Kamati ya uchunguzi  imeonyesha mapungufu na ukiukaji wa Maadili ya kiutumishi na kupendekeza tuhuma hizo zifikishwe Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM kwa hatua zaidi.

Ndugu Sixtus Rapheal Mapunda Baraza limebaini mambo yafuatayo:

Kuchukua Hati ya UVCCM bila idhini ya kikao husika. Hakutoa taarifa rasmi kwa Mwenyekiti au kikao cha Kamati ya Utekelezaji Taifa kuhusu maombi ya UVCCM Mkoa wa Iringa ya kubadilisha  matumizi ya eneo.

Hakutoa taarifa ingawa kulikuwa na vikao vingi vya Kamati ya Utekelezaji na sekretariet kuhusu shamba la Igumbilo.

Alipokea fedha za mgao wa mauzo toka kwa aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa Ali Nyawenga

Kutojibu barua ya maombi kutoka Mkoa wa Iringa kwa maandishi japokuwa barua zililetwa Makao Makuu.

Kuamua kupeleka Hati ya shamba Mkoani Iringa bila vikao vya maamuzi kuvishiriskisha na kuamua.

Alishindwa kutimiza wajibu wake kikanuni kwa kutosimamia majukumu yake ya kila siku akiwa na dhamana ya Katibu Mkuu.

Kuna upotevu mkubwa wa nyaraka husika ndani ya Ofisi yake wakati akiwa na wadhifa wa Katiba Mkuu.

Kutumia vibaya madaraka aliokuwa hayo, akiwashawishi walio chini yake kuvunja kanuni na taratibu za CCM pamoja na kuihujumu jumuiya na mali zake akiwa na dhama ya Katibu Mkuu wa UVCCM huku akiwa na dhamana ya usimamizi na utunzaji Mali za Jumuiya.

 Baraza Kuu la UVCCM  Taifa limeamua baada ya kuona kuna ukiukaji wa Maadili na taratibu uliosababisha sakata la shamba huko  Igumbilo, tuhuma hizo dhidi yake zifikishwe kwa Katibu Mkuu wa CCM kwa hatua zaidi.

Ndugu Suhail Ismail Baraza Baraza Kuu la UVCCM Taifa limeamua juu ya eneo alilouziwa kimakosa na Viongozi wa UVCCM Mkoa wa Iringa ambalo analimiliki Kisheria (ana Hati halali) ya eneo hilo lenye viwanja 25.

Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa limeamua kurudisha umiliki wa eneo hilo Kisheria.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunawaomba tunawashauri na tunasisitiza kwa Chama Cha Mapinduzi watimize wajibu wao katika kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wale wote waliohusika na kadhia hii ambao wako kwenye mamlaka yao ili kurudisha heshima na nidhamu ya Chama.

Ndugu Waandishi wa habari

Umoja wa Vijana wa CCM kuanzia mwezi wa Desemba, 2015 ulianza kujitathimini na kuweka mikakati ya kufanya mabadiliko ya kimfumo, kiutawala na kiuendeshaji ili kukidhi haja ya muda tulionao katika kuiongoza Taasisi hii kitaalamu zaidi.

Umoja wa Vijana iliunda Kamati ndogo ndogo kutathimini miradi yake ambayo ilionekana kuna upotevu mkubwa wa fedha za Jumuiya kama ifuatavyo:-

Kinondoni
Malipo ya mafao ya Watumishi (NSSF)
Kupitia migogoro ya ucheleweshaji wa utekelezaji mikataba mbalimbali na kadhalika.

Ripoti za Kamati hizo zinaendelea kufanyiwa kazi hatua kwa hatua. Katika Hatua ya awali  Umoja wa Vijana wa CCM uliomba kwa Katibu Mkuu wa CCM  kupatiwa wakaguzi wa hesabu ili kukagua miradi yote ya UVCCM Taifa. Awamu ya kwanza ya  ukaguzi umeanza katika miradi ya:

Majengo pacha ya uwekezaji Makao Makuu Dar es Salaam

Mradi wa Uwekezaji wa Vibanda vya Kinondoni

Kukagua matumizi ya Malipo mbali mbali (Watumishi, Mishahara na shughuli zote za Utawala)

Awamu ya pili ukaguzi wa hesabu  unaendelea katika miradi wa Uwekezaji Darajani Zanzibar
Mradi wa  Gymkhana Zanzibar
Shamba la Vijana Tunguu
Shamba la Vijana Ihemi
Matumizi ya Mkutano Maalum wa ushirikiano kati ya UVCCM na nchi rafiki uliofanyika Arusha
Miradi yote midogo midogo

Sambamba na hilo UVCCM inaendelea na zoezi la uhakiki wa watumishi wake wote na Mali zake ngazi ya Taifa hadi Wilaya na baada ya kukamilika ripoti zote zitawasilishwa kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

Ndugu Waandishi wa Habari

Mwisho kwa upande wa Baraza la kuu  UVCCM Taifa kwa ujumla liliazimia yafuatayo:

 Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, tunampongeza Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli na Serikali yake kwa Kazi kubwa, Utendaji unaotia matumaini wenye lengo la kuwahudumia wote bila ya kujali itikadi za kisiasa, rangi, kabila au jinsia.

2. Baraza Kuu la UVCCM , tunaiagiza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, kupitia Wizara yenye dhamana, itenge maeneo maalum kwa ajili ya vijana ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji mali na biashara bila kupata  bughudha au usumbufu wowote.

Baraza Kuu la UVCCM Taifa tunaigiza serikali kwamba, Halmashauri yoyote nchini ambayo itashindwa kutoa asilimia 5 ya Mapato yatokanayo na Vyanzo vya Mapato kwa makundi ya Wanawake na Vijana katika mpango wa kuwapatia mikopo, ipewe Hati chafu ili kuzihimiza Halmashauri nyingine kutambua umuhimu wa kutenga asilimia 5.

Aidha Baraza Kuu la UVCCM, limewaagiza Viongozi wa Jumuiya hiyo katika ngazi zote nchini, wasikilize kero za Vijana, kusaidia katika kukabiliana nazo na kuziwakilisha katika ngazi husika kwa ajili ya kuzitafutia  utatuzi. Aidha viongozi wote wawe karibu na vijana katika maeneo yao kwa dhumuni la kubaini kwa haraka changamoto zinazowakabili na kuwatatiza.

 Baraza kuu la UVCCM, tunatoa wito kwa viongozi wote kuwahamasisha vijana ili wajiunge katika vikundi na kufuata taratibu za kisheria ili kupata usajili, wawasimamie ili kufungua Akaunti Benki hatimaye fedha zitakazotolewa na serikali kwa ajili ya kupatiwa mikopo ziende kwenye vikundi hivyo na kuwa rahisi kukopesheka hususan baada ya kupata elimu ya mikopo na ujasiriamali.

Baraza kuu la UVCCM liamizia mali zote za jumuiya zikaguliwe zitambuliwe na zioneshe jinsi zinavyonufaisha taasisi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


Shaka Hamdu Shaka (MNEC)

KAIMU KATIBU MKUU
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment