UVCCM WAENDELEA KUVUANA NGUO HADHARANI...
TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA KWA VYOMBO VYA HABARI ILIOTOLEWA NA KAIMU KATIBU MKUU SHAKA HAMDU SHAKA KWA WAANDISHI WA HABARI AGOSTI 13 MWAKA 2016 JIJINI DAR ES SALAAM.

Baina ya tarehe  12  na 16 Agosti mwaka huu  mtu mmoja  anayejiita kada na mwanachama wa CCM  amekutana na vyombo vya habari pia akasambaza taarifa yake  katika mitandao ya kijamii akielezea msuala kadhaa ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake lakini zaidi akionekana kwa dhamira na makusudi bayana akiilenga Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya CCM  huku akiwa hana nguvu ya hoja.
Kwanini tunasema hakuwa na nguvu ya hoja zaidi ya kubwabwaja kichwa mchungwa   kuliko uthabibiti wa matamshi yake katika kujenga hoja zenye mantiki, ushahidi, kuwa na maana au mashiko ili kuyapa nguvu  madai yake na uthibitisho kamili juu ya anachokisema huku akiitaja UVCCM.
Kama kweli  ni mwanaccm au mwana jumuiya au ni  mtendaji dhamana wa jumuiya yetu, alipaswa kufuata taratibu na si kama alivyoamua kujipa dhamana bandia ya kuupotosha umma kwa kupiigania maslahi binafsi ya tumbo lake.
Aidha sote kama tujuavyo ni kwamba Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake zimeundwa kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu zake husika .Uamuzi wa kiongozi au mwanachama  kusimama hadharani na kukishambulia Chama au jumuiya hasa katika masuala mazito ya ufisadi ni jambo linalohitaji kwanza mtoa hoja awe na ushahidi wa kutosha, vielelezo na viambatanisho vya madai yake .
Ikiwa kila mwanachama akiamua akimua kuamka kitandani ,  kujipachika wadhifa wa ukada baadae  akakukutana na wanandshi wa habari kutoa shutuma, lawama na tuhuma , huo si mfumo bora na utaratibu wa chama chetu wala  jumuiya zake.
Matamshi ya mtu aliyejiita kada  yanayomtaka Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Magufuli aunde Tume ya Uchunguzi wa Mali za Jumuiya ya Umoja wa Vijana kwani Hali yake ni Mbaya Juu ya Mambo yafuatayo
1. Mapato ya Jengo na Juu ya Matumizi ya Fedha zinazopatikana na Mapato hayo ikiwa ni Mradi mkubwa wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM ).

2. Minada Holela ya Mali za Chama ikiwemo Magari n.k.ambayo imekua ikifanyika kinyume na Taratibu.

3.Uhakiki wa mali za jumuiya katika miradi ya Gymkhana na Darajani zanzibar

4.Kushughulikia Wasaliti ndani ya Chama na Jumuiya yetu ya UVCCM ambao wamekua mchana CCM usiku vyama vya upinzani.

Kimsingi madai yote haya ni mazito mno, kutokanana na unyeti pia uzito tuhuma husika , watu wengi walitegemea kama kweli angekuwa ni  muungwana, kwanza angefuata utaratibu na angeonyesha ushahidi , vielelezo au viambatanisho vya tuhuma hizo moja baadae ya moja kwasababu madai hayo ni mzingo wa  jinai.
Ninachokisema ni kwamba  chama chetu na jumuiya zake zimeundwa kwa  taratibu halali na husika za katiba , viongozi wa jumuiya na chama si mazuzu wa kupuuzia au kushindwa kusimamia dhamana na wajibu walionao au kushindwa kuyatolea maelezo na majibu sahihi au  yakinifu madai yote yanayoweza kujitokeza .
Kwa bahati mbaya sana utaratibu anaoutaka mtu aliyejiita mwanachama na kada unaweza kufanyika kwenye vyama vingine ambavyo naamini baadhi yake havina Katiba, Kanuni na havifuati miiko ma maadili waliojiw... read more

SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment