Shirika la ndege Marekani Delta lasitisha safari zake

Shirika la ndege Marekani, la Delta, limetangaza kusitisha na kuchelewesha safari zake baada ya kutokea matatizo ya mfumo wa komputa wa ndege zake kote duniani.

Delta imesitisha tena safari baada ya kukatisha safari zake siku ya jumatatu na kuwaacha maelfu ya wasafiri wakihangaika.
Baadhi ya abiria waliokwama
Image captionBaadhi ya abiria waliokwama
kushindwa kwa mfumo wa komputa wa kampuni hiyo ulisababishwa na kukatika kwa umeme katika makao mkuu mjini Atlanta.
Delta imesitisha tena safari baada ya kukatisha safari zake siku ya jumatatu
Image captionDelta imesitisha tena safari baada ya kukatisha safari zake siku ya jumatatu
Shirika hilo la Delta limesema kuwa abiria waliositishiwa safari au kucheleweshwa watapewa ndege nyingine au kurudishiwa gharama zao.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment