MTANZANIA ALIYEAHIKA NAFASI YA 5 KATIKA RIADHA RIO 2016 AFUFUA MCHEZO WA RIADHA TANZANIA MAKAMPUNI YAMGOMBEA KUMPA MIKATABA MINONO.

​RAIS WA SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA​ - ​ANTHONY MTAKA​ ​AKISHUHUDIA MKATABA WA MWANARIADHA​ - ​ALPHONCE FELIX SIMBU NA KAMPUNI YA MULT CHOICE​  ​DSTV​- ​TANZANIA​

Alphonce Felix Simbu ni Mwanariadha wa Tanzania ambaye alishika nafasi ya Tano  katika mbio ndefu za Marathon wakati wa Mashindano ya Olympic yaliyomalizika Mwaka huu RIO Nchini Brazil.

Mkataba huo umesainiwa mbele ya mkurugenzi mtendaji wa Mult Choice Tanzania ​Ndugu Maharage Chande​ na Meneja masoko ​Bi.Furaha Samalu​ na kushuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ndugu ​Anthony Mtaka​ ambapo kampuni ya Mult Choice Tanzania imemteua mwanariadha Alphonce Felix Simbu kuwa ​"Brand Ambasador"​ wake kwa Mkataba wa Shilingi Milioni Moja kwa Mwezi kwa Mda wa Mwaka Mmoja

Mungu ambariki Katika Safari yake ya Michezo.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment