MAKONDA AKUTANA NA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA (FFU)UKONGA
MAKONDA AKUTANA NA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA  (FFU)UKONGA
-Awapongeza kwa Uzalendo wao Kwa Taifa letu .

-Awaahidi kuwapatia Ambulance 

-Awataka Waifanye Dar Kama Dubai Kiulinzi. 

  Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh.Paul Makonda Leo amekutana na kikosi cha kutuliza ghasia(FFU)ukonga Jijini Dar na amezungumza  mengi moja kubwa nao ni Mhe. Makonda amewaeleza kuwa hakuna wafanyakazi wazalendo kama Askari kwani wao wako tayari kufa ili taifa letu Liwe salama.     Makonda aliongezea kwakusema uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua  uhai wa mtu.Rc Makonda amewaahidi kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba wafanye dar iwe kama dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta.  Rc.Makonda anaamini dar inapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa. 
Mwisho Mh.Makonda amewahakikishia askari hao wa FFU ukonga kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie askari katika hospitali yao huku akiahidi kufatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais Dkt.John Magufuli, ombi la Makonda lilikua     juu ya asilimia 20% ya faini zinazotozwa na trafiki zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji ikiwa pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili polisi watakapohitajika wawe wanafika bila kuchelewa.


SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment