.....KUMBE LOWASSA NA KINANA LAO MOJA NA HAWAJAKUTANA BARABARANI...? SOMA UNDANI WAKE >>>>>


LOWASSA NA MAGUFULI WATOA SOMO LA KISIASA KWA WATANZANIA WADHIHIRISHA SIASA SIO UADUI.

UKOMAVU WA KISIASA WA LOWASSA SASA KUWALAINISHA UKUTA SEPTEMBER 1..

Siasa ni tofauti ya hoja na mitazamo katika majukwaa ya kisiasa, siasa sio uadui na visasi.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana kwa bashasha na kupeana mikono na Edward Lowassa aliyekuwa mgombea Urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Picha hii imeenea sana kwenye mitandao ya kijamii wengi wakiielezea kuwa ni ishara ya  ukomavu wa kisiasa na pia ni funzo kwa wanasiasa wengine kuwa Siasa ni tofauti ya hoja na mitazamo kwenye majukwaa ya kisiasa lakini siasa sio kuendekeza uadui na visasi.

Rais John Magufuli na Edward Lowassa walichuana vikali sana katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015. Ushindani baina yao uliandika historia mpya katika siasa za Tanzania tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Edward Lowassa aliyekuwa kada wa muda mrefu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kupata nafasi ya kuhudumu Serikalini kwa nafasi mbalimbali ikiwemo Uwaziri na nafasi nyeti ya Uwaziri Mkuu alifanya uamuzi wa kihistoria kuhama chama tawala cha CCM na kuhamia chama cha upinzani cha Chadema. 

Tukio hilo la kihistoria lilibadilisha mtazamo katika siasa za Tanzania na kuzidisha ushindani wa kisiasa ambapo matokeo ya mwisho yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yalimpa ushindi Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kwa kura 8,882,935 huku mshindani wake kisiasa Edward Ngoyai Lowassa akipata kura 6,072,848. Hakika ulikuwa ni uchaguzi uliokuwa na ushindani wa aina yake na ni uchaguzi ulioacha historia.

Tangu wakati huo wawili hawa hawakuwahi kukutana hadharani mpaka leo walipokutana wakiwa wote ni waalikwa katika maadhisho ya Jubilei ya Dhahabu (Miaka 50) ya Ndoa ya Rais mstaafu wa awamu ya Tatu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Benjamin William Mkapa na mkewe Anna Mkapa iliyofanyika katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro eneo la Namanga jijini Dar es Salaam. 

Tukio hili la kukutana na kupeana mikono kwa kwa bashasha linaacha somo kubwa kwa wanasiasa wa Tanzania na watanzania kwa ujumla kuelewa kuwa siasa haipaswi kugeuzwa kuwa ni uadui na muendelezo wa visasi bali siasa ni utofauti wa hoja, ni utofauti wa mitazamo katika majukwaa ya kisiasa lakini pale inapotokea shughuli za kijamii kama hafla, misiba n.k

Wanasiasa waliokomaa kisiasa huweka kando tofauti zao na kuhimiza misingi ya Umoja na Mshikamano.

Katika hilo Rais Joseph Magufuli na Edward Ngoyay lowassa wamedhihirisha ukomavu wao.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment