Kenya yaendelea kutesa katika riadha duniani yashinda dhahabu mbio ya mita 3000 kuruka viunzi na maji


Conseslus Kipruto aliyeishindia kenya medali ya dhahabu
Image captionConseslus Kipruto aliyeishindia kenya medali ya dhahabu
Mwanariadha wa Kenya Conseslus Kipruto ameishindia kenya dhahabu ya nne katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji katika michezo ya Olimpiki inayoendelea mjini Rio.
Mwanariadha wa Marekani Even Jager alikuwa wa pili na kujizolea medali ya fedha huku bingwa mara mbili wa michezo ya Olimpiki Ezekiel Kemboi akichukua nafasi ya tatu na kuishindia medali ya shaba Kenya.
Kenya imekuwa ikijishindia medali ya dhahabu katika mbio hiyo tangu mwaka 1994.Kenya imejishindi medali mbili za dhahabu siku ya Jumatano baada ya Faith Kipyegon kuibuka mshindi katika mbio za mita 1,500 upande wa wanawake.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment