JACQUELINE MENGI AUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM KWA KUKARABATI NA KUNUNU VITABU VYA MAKTABA


JACQUELINE MENGI AUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM KWA KUKARABATI NA KUNUNU VITABU VYA MAKTABA

 Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (wa pili kushoto) akiwa ameongoza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (kushoto), Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge (wa tatu kushoto) pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kinondoni ambapo aliwahimiza kusoma kwa bidii vitabu hivyo ili kupanua ufahamu wao zaidi na hata kimasomo pia vitasaidia kuinua viwango vyao vya ufaulu.
 Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi na uongozi wa shule hiyo kwa pamoja wakiimba na wanafunzi wa shule ya Msingi Kinondoni.
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa maktaba ya vitabu aliyoipa jina la Dr. Ntuyabaliwe Foundation katika hatua za kumuenzi marehemu baba yake ambaye aliyemjengea misingi mizuri ya usomaji wa vitabu wakati wa makuzi yake
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akionyesha  wageni waalikwa picha mbalimbali za awali kabla ya kukarabati maktaba hiyo.

  Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maktaba ya Shule ya Msingi Kinondoni jijini Dar es Salaam.  Wanaoshuhudia tukio hilo ni Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (katikati) pamoja na Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge.
 Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi kwa pamoja wakizundua nembo ya taasisi hiyo.
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi wakipeana mikono na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda.
  Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akimwonyesha baadhi ya vitabu Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda vinavyopatikana katika maktaba hiyo.
Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akifurahi katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule hiyo wakati akiondoka shuleni hapo.

Na Mwandishi wetu
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa kizazi cha sasa na baadae, Jacqueline Mengi kupitia Taasisi yake ya Dk. Ntuyabaliwe ameamua kuunganisha nguvu kwa serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais Magufuli kwa kusaidia kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa kufanya marekebisho ya maktaba katika shule ya msingi Kinondoni.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo ambao uliambatana na uzinduzi wa Taasisi ya Dk. Ntuyabaliwe, Jacqueline amesaidia kufanya ukukarabati wa maktaba katika shule hiyo na kuweka vitabu ikiwa ni sehemu ya kumkumbuka baba yake Dk. Ntuyabaliwe kutokana na kupenda kwake kusoma vitabu.
Alisema baba yake alikuwa akiamini zaidi katika vitabu hivyo alipenda hata watoto wake wasome vitabu na anachokifanya yeye kwa sasa ni kuendeleza juhudi ambazo alikuwa akiifanya baba yake ya kuona watu wakisoma vitabu na matarajio yake ni kuona vitabu hivyo vikiwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kuwaongezea uwezo wa kufaulu katika masomo yao ya darasani.
"Ndoto yangu ya muda mrefu leo imetimia, kila mtu ambaye alikuwa akimfahamu baba yangu Dk. Ntuyabaliwe alikuwa akifahamu kuwa alikuwa anapenda vitabu na hata sisi alituzoesha kusoma vitabu na hata kuanzishwa kwa taasisi hii ni sehemu ya kumkumbuka yeye,
"Naamini kuwa usomaji wa vitabu unaweza kumsaidia mtu kufika mbali hata kama sio katika elimu unaweza kumsaidia kwa jambo lingine hata katika maisha ... ndoto yangu ni kuona watanzania wote wanapenda kusoma kama baba yangu alivyokuwa anapenda kusoma vitabu," alisema Jacqueline.
Nae mgeni rasmi katika shughuli hiyo, Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda alisema sio jambo rahisi serikali kuweza kumaliza changamoto zote zilizopo na kupitia watu wenye moyo kama wa Jacqueline ambao wanaunga mkono juhudi za serikali kunaweza saidia upatikanaji wa elimu bora.
Alisema kupitia maktaba hiyo anaamini ipo siku kutatokea mtu ambaye atakuwa na msaada kwa Tanzania ambaye wakati akisoma alikuwa akitumia maktaba ambayo imefanyiwa ukarabati na Jacqueline Mengi.
"Nimeona hali ambayo ilikuwa awali katika eneo hili na niseme tu Jacqueline atakuwa na yeye aliguswa na hali hiyo na nitumie fursa hii kumshukuru sana kwa msaada ambao ameutoa, shule inatakiwa kutoa elimu bora lakini ili kufikia malengo hayo kunahitajika kuwe na nyenzo za kutosha ambazo zitasaidia malengo ya kielimu kufikiwa," alisema Mapunda.
Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga alimshukuru Jacqueline Mengi kwa msadaa wa kukarabati maktaba ya vitabu ili wanafunzi kujisomea, maktaba ambayo awali hawakuwahi kuwa nayo.
"Tunakushukuru sana kwa maktaba hii sasa wanafunzi wataweza kujisomea, tunafahamu juhudi za Dk. Mengi katika kusaidia elimu kwa kutoa madawati sasa na wewe umemuunga mkono tunawashukuru kwa hilo," alisema Ntenga.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment