HAYATT AL HAJJ ABOUD JUMBE MWINYI AONDOKA NA KUWAACHIA WANA WA NCHI YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR WOSIA MZITO... WASIPOUTEKELEZA........
WOSIA WA ALHAJ ABOUD JUMBE.

ENYI wenye kuamini, mcheni Mwenyenzi Mungu vile ipasavyo waja kumcha, wala msife ila ilhali ni miongoni mwa Waislamu. (Imran 101).

Mimi, Aboud Jumbe Mwinyi, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunibariki kuzaliwa ndani ya Uislamu, na namuomba aniruzuku kufa na kufufuliwa ndani ya Uislamu. Katika hali zote hizo inampasa mja awe wote ndani ya Uislamu kama iagizavyo aya ifuatayo:

"Enyi mlioamini, ingieni kikamilifu mnamo hukumu zote za Islamu"

"Wala msifuate nyayo za shetani, kwani yeye ni adui aliye dhahiri". (Baqarah 208)

Hivyo, ni matumaini yangu kwamba kama Mwenyezi Mungu alivyonirehemu kuwa Muislamu, atanijaalia nikifa kukoshwa, kukafiniwa, kuvishwa sanda, kutiwa katika jeneza, kusaliwa na kuzikwa kwa mujibu wa Sunna ya Mtume Muhammad (s.a.w.). Agizo hili si ombi bali ni haki yangu kama binadamu, kama ni Muislamu, na kama ni Mtanzania.

Haki ya Uhuru wa kuabudu inaelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo vifungu vifuatavyo:

19(1) Kila mtu atakuwa na haki na uhuru wa mawazo (fikra), imani na haki ya kuchagua kuhusu dini aitakayo, pamoja na uhuru wa kubadili dini au imani yake.

19(2) Bila kuathiri sheria zilizoko za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, shughuli za dini, za kuabudu na kueneza dini zitakuwa huru na ni jambo la khiari ya mtu nafsi yake na uendeshwaji, uendelezwaji shughuli za dini na vyombo vya dini kamwe hazitakuwa sehemu za serikali.

Kwa ufunguzi wa wasia huu, maana ya kuumbwa mauti na maisha, sababu na lengo lake ni kutufanyia mtihani ni nani miongoni mwetu ni mwenye vitendo vizuri zaidi. Nikiwa hai, dhamana ya vitendo vyangu vinaniangukia mimi mwenyewe, nikifa dhamana, ikiwa vitendo vyema au vibaya nitakavyofanyiwa itawaangukia waandalizi, watendaji na wenye kushiriki katika vitendo hivyo, na Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu na mwenye msahama. SITAKI katika maziko yangu kutumbukizwa chochote kiendacho hata kidogo kinyume na mafundisho ya Islamu. SITAKI beni, SITAKI mizinga, SITAKI maombolezo wala lolote lingine lenye hata chembe ya kufuru. SITAKI hivyo nikiwa hai, nitakapoondoka katika dunia Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi wangu, duniani na akhera.

Wassalamu Alaykum Warahmatu Llahi wa Barakaatuh.

Aboud Jumbe Mwinyi

Nakala:
Mufti wa Zanzibar
Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Mwanasheria Mkuu
Sharrif Abdul Qader Juneiyd
Sheikh Nurudeen Hussein
Sheikh Mzee
Prof. Juma Mikidadi
Wanangu.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment