Guinea: Wanaotaka kwenda kuhiji Mecca wakwama


MeccaImage copyrightAFP
Image captionHija ni tukio la kila mwaka
Kundi la Waislamu wa Guinea waliolipa nauli ya kwenda Mecca kwa ajili ya Hija ya mwaka huu limekwama katika kituo kikuu cha waislam katika mji mkuu, Conakry, huku wakisubiri kupewa Visa ya kwenda Saudi Arabia.
Takriban raia 7,200 wa Guinea walijisajiri kuhudhuria hija wakilipa karibu dola $5,000 kwa ajili ya safari hiyo, lakini nyingi kati ya visa zao bado hazijatolewa.
Mmoja wa mahujaji, Aboubacar Sow, anasema aliambiwa kwamba ataondoka Jumatatu.
Ni siku tatu sasa sijaoga. Hata kupata maji ya kutawaza kabla ya kusali hakuna. Hatujui nini kinaendelea kuhusu safari yetu.
Lakini bado hana paspoti na amekwama katika kituo cha Waislam kwasababu alisafiri kutoka Labe, umbali wa kilometa 300km, kwa ajili ya safari hiyo.
Muhujaji mwingine aliiambia BBC kwamba visa zimekuwa zikija moja baada ya nyingine baada ya muda na ni watu wachache ambao wamepelekwa uwanja wa ndege.
Kwa miaka miwili iliyopita, raia wa Guinea walipigwa marufuku kwenda Hija kwasababu ya mlipuko wa Ebola.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment