CHARLES KITWANGA UMECHELEWA SANA, UMEKUMBUKA SHUKA KUMEKUCHA UMEONYESHA SURA HALISI YA ‘UNAFIKI’ WA WALIO WENGI SERIKALINI.Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani Charles Kitwanga.
CHARLES KITWANGA UMECHELEWA SANA, UMEKUMBUKA SHUKA KUMEKUCHA UMEONYESHA SURA HALISI YA ‘UNAFIKI’ WA WALIO WENGI SERIKALINI.
Na Comrade Sambala.
WhatsApp +255625567647.

Nami ni mmoja walisoma na kuelewa maoni ya aiyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga kuhusu makosa yaliyofanyika katika kununua ndege za shirikia la ndege la Tanzania ATCL,

Katika maoni yake yaliyonukuliwa ana vyombo vya habari na mitandao kijamii, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ameziponda ndege mpya za ATCL. Amesema hazina mwendo na zimetoka katika kampuni ndogo ya mtu binafsi, na amehoji ubora wake.

Kitwanga akaongeza usema kuwa ni ajabu kununuliwa kwa fedha taslimu wakati duniani kote ndege hununuliwa kwa kulipa kidogo kidogo wakati mteja akiendelea kuzitumia.

Kama ni kweli tumenunua ndege ‘Cash Money’ ,Basi walioenda kunegotiate deal huenda hawana uzoefu, kwani hata Emirates wananunua kwa Installments, nadhani hata Bombadier hawajatutendea haki pia kwa kuwa hata wao wanajuwa wateja wao wote wanalipia kidogo kidogo. 


Tungeweza kutumia hiyo pesa kama advance Payments ya ndege kumi ...kwa mikataba ya Ndege mbili Kila mwaka kwa miaka mitano Sijashangaa kuona Gazeti La Leo Nipashe Charles Kitwanga akishangaa naye ndege kununuliwa cash( full payment) serikali haijachelewa iombe mkataba uboreshwe ili hayo malipo yawe advance ya ndege 10 kwa miaka mitano.


Hayo ni makosa makubwa ambayo yanalitafuna taifa na bahati mbaya sana haya hayafanywi na viumbe wengine isipouwa sisi binadamu na tena Viongozi wa serikali waliopewa dhamani ya kusimamia taifa letu.

Lakini kwa upande wangu nami namponda na kumshangaa sana Kitwanga manake mpaka tarehe 20 mwezi mei alikuwa bado waziri wa mambo ya ndani na ‘alishiriki Vikao vya baraza la mawaziri’
,
Na mipango ya kununua ndege haikuja siku moja ilianza kujadaliwa toka Mh Rais Dk Magufuli anaingia madaraka na watalamu wa masuala ya usafirishaji wa anga kupitia wizara husika ‘walipeleka mchakato wote baraza la mawaziri ili kupata baraka za mwisho kutekeleza’,

Swali la kujiuliza je Kitwanga alikuwa wapi kushauri aina ya ndege na namna ya kuzinunua...? kwa nini mda wote walikaa kimya na kubaki kuimba na kusifu kila sauti waisikikiayo bila kushauri na leo analalamia kuwa tumekosea kununua ndege zile.

Pia namfananisha kitwanga na walioshangilia kuhamia Dodoma mpaka baadhi ya mawaziri wakajipa siku 14 kuwa watakuwa dodoma bila kuangalia uhalisia na maelekezo ya Mh rais alisema ndani ya miaka minne wawe tayari Dodoma.

Nawaomba sana viongozi wangu mliopewa dhamani ya kuongoza taifa hili msaidieni na mumshauri vyema Mh Rais ili kulisiadia taifa katika mambo ya msingi badala ya kulalamika maamuzi ambayo nyie ni sehemu ya hayo maamuzi.

Binafsi naunga mkono mambo yote ya msingi anayofanya mh rais iliwemo la kufufua shiria la ndege na kufanya mageuzi makubwa katia mifumo yote ya utawala kama anavyofanya sasa, (Japo nilitamani sana kulivunja shirika la ndege la sasa ATCL na uanzisha KILIMANJARO AIRWAYS) Kisaikologia matatizo ya ATCL huko nyuma bado yapo vichwani mwa watu.


Taifa hili litajengwa na wenye moyo na uliwa na wenye meno.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment