BREAKING NEEWS-:NAIBU WAZIRI ELIMU MANYANYA ATUMBUA JIPU MKOANI SIMIYU-

BREAKING NEEWS-:NAIBU WAZIRI ELIMU  MANYANYA ATUMBUA JIPU MKOANI SIMIYU-
Mheshimiwa Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi-Injinia Stella Manyanya  amemuondoa katika nafasi yake aliyekuwa kaimu mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi-BUNAMHALA -FDC-Kilichopo wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu ndugu Ramadhani Makolo na kumteua Bi.Levina Mrema kuwa kaimu mkuu wa chuo hicho wakati wizara ya elimu ikijipanga katika kukiboreshea miundombinu yake,kabla ya uteuzi huo Bi.Levina alikuwa mkuu wa idara ya fedha na mipango katika chuo hicho,Mh.Manyanya amefikia maamuzi hayo baada ya kutoridhishwa na maelezo ya aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo Bwana Ramadhani Makolo-Katika ziara hiyo naibu waziri alijionea miundombinu chakavu ya chuo hicho huku kukiwa na watumishi kumi ambao wamekuwa wakipokea mshahara bila kuwa na kazi yoyote wanayoifanya chuoni hapo,chuo hicho kimepokea wanafunzi nane tu kwa mwaka huu jambo ambalo Mh.Naibu waziri hakuonyesha kuridhika nalo,katika ziara hiyo ambayo Naibu waziri aliambatana na maafisa wa Veta kanda ya Magharibi ameahidi kutoa kiasi cha sh.Milioni saba,sh.Milioni tano zikiwa za ukarabati wa bweni na sh. milioni mbili zikiwa za kusaidia vijana katika ujasiliamali akiutaka uongozi wa chuo hicho kubuni miradi na mafunzo ya ujasiliamali itakayoendana na soko la sasa.Mh.Manyanya yupo katika ziara yake ya kikazi katika mikoa mbalimbali akijionea utekelezaji wa shughuli zilizo chini ya wizara ya elimu,Akiwa mkoani Simiyu Mh. Manyanya alipata pia nafasi ya kukagua eneo litakalojengwa Chuo Cha Ufundi Veta mkoa wa simiyu na kuahidi ujenzi huo kuanza mapema mwaka huu.

SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments: