WHITEDENT YASHEREHEKEA MIAKA 25 YA MAFANIKIO NCHI NZIMA.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akizungumza wakati wa kampuni ya Whitedent wakisherekea miaka 25 ya kutengeneza bidhaa za meno.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akiweka maboksi ya Whitedent wakati wa kuzindua shindano la whitedent linaloshindanishwa nchi nzima.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akiteta jambo na kiongozi wa Kampuni ya Whitedent Mkoani Tabora.

 Kampuni bidhaa za afya ya mdomo Whitedent inasherehekea kuadhimisha miaka 25 ya biashara kwa kufanya promosheni ya miezi mitatu ambapo watu nchini kote wananafasi ya kujishindia moja ya magari 25 ya aina ya Suzuki Alto K10. 

Whitedent inatoa nafasi kwa maelfu ya wananchi kushiriki shindano hili kwa kukisia idadi ya pakiti za whitedent zilizomo ndani ya moja ya magari hayo ya Suzuki litakalokuwa linazunguka nchi nzima wakati wa promosheni. Mteja atatakiwa tu kujaza fomu ya ushiriki katika kipindi hicho cha promosheni na kukisia jibu sahihi ili aweze kuingia katika droo kubwa ya kujishindia moja ya magari hayo ya Suzuki Alto 10 mwisho wa promosheni hii Oktoba mwaka huu.  

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa promosheni, Afisa Mkuu wa Chemi & Cotex Raja Swaminathan alisema, “Katika kusherehekea miaka 25 ya bidhaa hii tumetaka kuwashirikisha wananchi wote katika mafanikio yetu. Tunatoa magari haya ambayo ni mapya kabisa yakiwa yamejaa mafuta kwenye tenki lake, na yakiwa yamelipiwa ushuru na bima kwa mwaka mzima. Katika promosheni hii, hakutakuwa na kiingilio cha aina yoyote na wala mshiriki hatakiwi kutumia hata shilingi moja ili aweze kushiriki na zaidi ya hapo watu wote wanaweza kushiriki mara nyingi wawezavyo.”

Shindano hili litakalokuwa chini ya uangalizi mkubwa na wa makini wa Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania itachukua miezi mitatu na itashirikisha mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar.

“Tungependa kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika shindano hili. Bidhaa ya Whitedent ni ya kujivunia ya Tanzania kwa Watanzania ikiwa imetengenezwa na Watanzania. Safari ya promosheni itapita sio mijini tu bali pia katika vijiji ili kuhakikisha kila mtu ana nafasi ya kushiriki,” aliongeza Swaminathan. 

Inakadiriwa kuwa zaidi ya wana Afrika Mashariki milioni 14 huanza siku yao kwa kupiga mswaki kwa kutumia Whitedent. Nchini Tanzania kupitia ukaguzi wa Nielsen wa mwaka 2012 ulionyesha kuwa Whitedent ina asilimia 79 ya soko nchini na hupatikana katika maduka makubwa ya bidhaa hadi kwenye vioski vidogo. 
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment