UTURUKI YAENDELEA KUSAFISHA JESHI LAKE NA KUWASAKA WAHIANI NI BAADA YA MAPINDUZI KUFELI

Image copyrightREUTERS
Image captionAskari walioshiriki katika mapinduzi wakiwa wamesalimu amri
Viongozi wa jumuiya ya umoja wa ulaya wameitaka Uturuki kuchukua hatua kwa muujibu wa sheria kufuatia jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa ambayo yalifanyika mnamo mwishoni mwa juma lililopita, kauli hiyo imekuja kufuatia hatua zinazoendelea kuchukuliwa na rais wa nchi hiyo Tayyip Erdogan kuwatimua kazi maelfu ya maafisa wa polisi.
Naye kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameionya nchi ya Uturuki juu ya nia yake ya kutaka kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya kuwa inaweza isifanikiwe endapo rais Edogan ataendelea kuikumbatia adhabu ya kifo na vitisho nchini mwake .
Marekani nayo imeitala Uturuki kuchukua hatua kwa muujibu wa sheria zilizopo.inakadiriwa watu wapatao elfu saba wako kizuizini na maelfu wengine kusimamishwa kazi wakiwemo majaji na maofisa wakuu jeshini
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment