URENO WATAWAZWA MABINGWA WAPYA WA ULAYA 2016 WACHUKUA UBUNGWA MBELE YA UFARANSA IKIWA NYUMBANI STADE DE FRANCE.

Ureno Wakishangilia ubingwa baada ya kukabidhiwa 'NDOO' yao kama mabingwa wapya Ulaya 2016

FURAHA YA USHINDI BAADA YA KUTWAA UBINGWA.
EderImage copyrightGETTY
Image captionEder akifunga bao la ushindi
Ureno wameshinda michuano ya kandanda ya Ulaya, Euro 2016, kwa kuwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika dakika za ziada kwenye mchezo wa fainali mjini Paris.
Goli la ushindi lilifungwa na Eder katika dakika ya 110, na kusababisha huzuni kubwa kwa mashabiki wa Ufaransa waliofurika kwenye uwanja wa Stade de France.
EderImage copyrightGETTY
Image captionEder asherehekea na wenzake baada ya kufunga
Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Ureno. Hii ni mara ya kwanza Ureno kushinda michuano mikubwa.
Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano bila ya mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo aliyetoka kutokana na kupata jeraha la goti katika kipindi cha kwanza.
Image copyrightAP
Ufaransa ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini hawakuweza kuzitumia vyema nafasi walizopata.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment