Sudan Kusini yakana barua ya kumkamata Machar

Image captionBarua bandia
Serikali ya Sudan Kusini imepuuzilia mbali barua bandia inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikiamrisha jeshi la taifa hilo kumkamata aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar akiwa hai ama akiwa amefariki.
Msemaji wa serikali alionekana katika runinga ya taifa na kutoa kile alichokitaja kuwa sababu saba kwa nini barua hiyo ni bandia ikiwemo ile ambayo inaenda kinyume na ukomeshaji wa uhasama uliokubalika.
Image copyrightAFP
Image captionRiek Machar na Salva Kiir
Barua hiyo haina nambari za uthibitisho,uhalisi wa saini mbali na muhuri wa 'siri' kama ilivyotarajiwa.
Mtu aliituma kanda ya video katika mtandao wa Facebook akiisoma taarifa hiyo.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment