SERIKALI ZA TANZANIA NA KOREA, ZATILIANA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Wizara ya Fedha ya Korea Weon-Kyoung Jo (kushoto) akizungumza wakati wa mjadala wa Ushirikiano katika misaada ya maendeleo ya kiuchumi kabla ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Korea, yenye thamani ya dola Milioni 300, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es salaam.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo baada ya kusainiwa. Hati hiyo ina thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakisaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakipeana mikono baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thmani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 300, katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.

Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta Mutagwaba, akipeana mkono na mmoja wa wajumbe kutoka Korea baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.

Wajumbe kutoka Serikali ya Korea wakisoma Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini na Serikali ya Korea kabla ya kusainiwa.

Wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia mjadala wa Ushirikiano katika Misaada ya Maendeleo ya Kiuchumi uliofuatiwa na kutiliana saini kwa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini.

Mjumbe kutoka Tanzania akichangia hoja katika mjadala wa Ushirikiano katika Misaada ya Maendeleo ya Kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara jijini Dar es salaam kati ya Tanzania na Korea, kabla ya kusainiwa kwa Hati ya Ushirikiano ambapo Korea imeahidi kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 650.

Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta  Mutagwaba (kulia) na wajumbe wengine wakifuatilia mjadala kuhusu Ushirikiano katika Misaada ya Maendeleo ya Kiuchumi kabla ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Hamis Shaban (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo (katikati) wakibadilishana mawazo baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, kulia ni Afisa kutoka Korea.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tanzania na Korea baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo .


Na Benny Mwaipaja,MoFP

SERIKALI za Tanzania na Korea Kusini, zimetiliana saini Hati ya Makubaliano (Aide Memoire) kwa ajili ya Ushirikiano wa utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa Maji, Nishati, Kilimo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHAMA na Viwanda itakayogharimu Dola za Marekani Milioni 300, sawa na TSh.Bilioni 650, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2016 hadi 2020.

Fedha hizo ni sawa na ongezeko la Dola Milioni 100 ikilinganishwa na kiasi cha Dola Milioni 200 ambazo nchi hiyo ya Korea iliipatia Tanzania kama mkopo wenye masharti nafuu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita (2014 hadi 2016).

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, ametia saini makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, huku upande wa Korea Kusini ukiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Korea Bw. Weon-Kyoung Jo.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ni mwanzo wa matayarisho ya kuandaa Mpango kazi wa namna ya kutekeleza miradi hiyo ili iende sambamba na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka 5 uliozinduliwa hivi karibuni mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Mkakati Mbadala wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA Successor Strategy).

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, amesema kuwa miradi hiyo ya maendeleo iliyochaguliwa kutekelezwa katika sekta zilizotajwa zitachochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na kupunguza umasikini kwa wananchi.

Bi. Amina Shaaban alisema kwamba Hati hiyo ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Korea Kusini, yamejikita zaidi katika uboreshaji wa mifumo ya Tehama, kuimarisha sekta ya kilimo pamoja na kuboresha miundombinu inayosaidia ukuaji wa viwanda hususan ya nishati ya umeme katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2020/21.

“Ushirikiano wa Tanzania na Korea Kusini umeanza tangu mwaka 2000, kwa kuhusisha taasisi zake mbili ambazo ni Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) ambalo limeipatia Tanzania kiasi cha zaidi ya dola za Marekani 30.9 na Benki ya Exim-Korea ambayo imetoa Dola za Marekani zaidi ya Milioni 455 sawa na zaidi ya Tsh 900 bilioni kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miaka 10 iliyopita” alisema Bi. Amina Shaaban

Ametoa wito kwa nchi hiyo kuwekeza hapa nchini kutokana na fursa mbalimbali zilizopo za kiuchumi zikiwemo mazingira mazuri ya uwekezaji, rasilimali za kutosha ikiwemo gesi asilia, madini, sekta ya utalii, hali nzuri ya hewa pamoja na amani na utulivu.

Akizungumza katika tukio hilo Weon-Kyoung Jo, amesema kuwa Tanzania inaongoza katika bara la Afrika kupata misaada na mikopo nafuu kutoka Korea Kusini baada ya nchi hiyo kuridhishwa na mipango mizuri ya maendeleo iliyowekwa na Serikali ya Tanzania.

Amesema kwamba vipaumbele vilivyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano zikiwemo Sekta za Viwanda, Kilimo na TEHAMA vinaungwa mkono na nchi yake na kwamba wako tayari kusaidia kwa njia ya kutoa ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda, Afrika Mashariki na Kimataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, amesema kuwa serikali ya Tanzania inatarajia kufungua ubalozi wake nchini Korea Kusini ili kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment