NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA UENDELEZAJI MILKI

 Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akifungua mkutano wa Wadau wa Uendelezaji Milki uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga jijini Dar es salaam kwa lengo la kuanzisha Chama chao kwa ajili ya kusimamia masula mbalimbali ya Uendelezaji wa Miliki , Moja ya mambo yaliyojadiliwa katika mkuta no huo ni Katiba Pendekezwa ya Chama hicho ambapo wajumbe wamepata muda wa kuchangia mawazo yao na kurekebisha baadhi ya vifungu ili kuipitisha mara baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akizungumzia masuala mbalimbali katika  mkutano wa Wadau wa Uendelezaji Milki uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga jijini Dar es salaam
 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula ili  akifungua mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu na Miliki Hamad Abdallah Mkurugenzi wa wakifuatilia kwa karibu wakati mkutano huo ukiendelea
 Baadhi ya wadau waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia kwa karibu masuala kadhaa ambayo yamezungumziwa katika mkutano huo.
 Mmoja wa wadau walioshiriki kwenye mkutano huo Bw. Emilian Rwejuna akiwa pamoja na wadau wengine.
 Mkurugenzi wa Milki Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Hamad Abdallah akifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwanasheria wa Shirika hilo Elias Mwashiuya hayupo pichani wakati akitoa mada kuhusu katiba ya chama hicho  katika mkutano huo
 Itandula Gambalagi Mkuu wa Mauzo NHC akisalimiana na Bw. Adam Jee ambaye pia alihudhuria katika mkutano huo kama mmoja wa wadau wa Uendelezaji Milki.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu wakifuatilia maelezo ya Mwanasheria wa NHC Bw.Elias Mwashiuya wakati alipokuwa akielezea vifungu mbalimbali kuhusu katiba ya chama hicho.
 Mwanasheria wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC akitoa maelezo kwa wadau wa Uendelezaji Milki kuhusu Katiba ya Chama hicho ambayo wadau wamepata fursa ya kuchangia mawazo yao kabla ya kupitishwa na chama hicho
 Wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo


Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa NHC Bw. Tuntufye Mwambusi, Hamad Abdallah Mkurugenzi wa Milki NHC, Suzan Omari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NHC na Mkuu wa Mauzo NHC Bw. Itandula Gambalagi wakiwa katika mkutano huo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment