MWENYEKITI WA CCM, RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA SEKRETARIETI NA KUZUNGUMZA NA WATUMISHI WA CCM - DODOMA​


Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli amekutana na Sekretarieti pamoja na kufanya mazungumzo na watumishi wa Chama cha Mapinduzi ofisi ya Makao Makuu Dodoma na watumishi kutoka Ofisi ndogo ya Lumumba jijini Dar es salaam katika ukumbi wa NEC uliopo Makao Makuu ya CCM, Dodoma.

Kikao hiko baina ya Mwenyekiti mpya wa CCM na Sekretarieti yake mpya aliyoiteua na kuthibitishwa  na Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 23/7/2016 ni Kikao cha kwanza cha utambulisho rasmi na kuweka mpango kazi.

Aidha, Mwenyekiti huyo wa CCM amekutana na watumishi wa CCM wa Ofisi ya Makao Makuu Dodoma na ofisi ndogo ya Lumumba, pamoja na kujitambulisha Dkt Magufuli ameahidi kushughulikia changamoto zote za utumishi ndani ya Chama, ameomba ushirikiano na kusisitiza kujituma na kufanya kazi kwa bidii.


SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment