Maalim Seif ‘afunguka’ viongozi wa CUF kukamatwa


Zanzibar. Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesikitishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi mbalimbali wa chama hicho katika ngazi za wilaya na majimbo.

Maalim Seif amesema hayo jana katika Baraza la Eid el Fitri lililofanyika katika ukumbi wa Wakfii wa Ngazija mjini hapa.

Amedai kuwa viongozi hao huwekwa ndani huku wakiteswa, kuadhibiwa na kulazimishwa kukubali kushiriki katika vitendo vya uhalifu ambavyo hawakuvitenda.

Hata hivyo, amesema  kuna mwendelezo wa kauli zinazoashiria azma ya kutaka kumkamata yeye, zinazotolewa na baadhi ya wakuu wa vyombo vya dola.

“Hakuna haja ya kuwatesa watu, iwapo wanayo azma ya kunikamata, mimi nipo waje tu wanikamate,” amesema Maalim Seif.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment