HIZI NDIO HABARI KUU ZILIZOGONGA VICHWA VYA HABARI DUNIANI LEO.. ZISOME HAPA ZOTE KUJUA MATUKIO MAKUBWA YA ELO DUNIANI.

Miongoni mwa habari nyingine kuu leo, Umoja wa Mataifa umehimiza pande zote kusitisha vita Sudan Kusini, na Korea Kaskazini ikaitahadharisha Marekani

Habari kuu ya leo Korea Kaskazini kujibu hatua ya Marekani

Image copyrightEPA
Jeshi la Korea kaskazini linasema litachukua hatua za nguvu dhidi ya kutumwa kwa mfumo wa hali ya juu kutoka Marekani kuzuia makombora angani Korea Kusini.
Limesema litachukua hatua punde litakapofahamu wakati na sehemu ambapo makombora hayo yatatumwa.
Maafisa Korea Kusini watadhibitisha katika wiki kadhaa sehemu ambapo makombora hayo yatatumwa.

1. Shangwe Ureno baada ya ushindi Euro 2016

Image copyrightGETTY
Sherehe zimetanda Ureno baada ya timu ya taifa ya kandanda kushinda ubingwa wa Ulaya kwa kuifunga Ufaransa bao 1-0 mjini Paris.
Mkusanyiko mkubwa wa watu wanacheza densi katika barabara za Lisbon.
Bao la ushindi lilifungwa na Eder kunako dakika za ziada, jambo lililowashangaza mashabiki wa nyumbani katika uga wa Stade de France.

2. UN yaomba viongozi kusitisha vita Sudan Kusini

Image copyright
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limewaomba viongozi wa kisiasa nchini Sudan kusini kudhibiti vikosi vyao vya kijeshi baada ya kuzuka mapigano katika mji mkuu Juba. Baraza hilo la usalama limeghadhabishwa na mashambulio katika makao ya Umoja wa mataifa na dhidi ya raia, likieleza huenda mashambulio hayo yakawa uhalifu wa kivita.

3. Shinzo Abe ashinda uchaguzi Japan

Image copyrightREUTERS
Matokeo ya mwisho katika uchaguzi wa jana nchini Japan yanaonyesha kuwa serikali ya muungano ya waziri mkuu, Shinzo Abe, umeshinda theluthi mbili iliyo muhimu katika bunge kuu.
Inampa bwana Abe nafasi ya kuikarabati katiba inayopinga vita nchini humo.

4. Mshambuliaji wa Dallas alipanga makubwa

MicahImage copyrightAFP
Image captionMicah Johnson
Mkuu wa polisi katika mji wa Dallas Marekani amesema mshambuliaji aliyewapiga risasi maafisa watano wa polisi na kuwaua, alikuwa anapanga shambulio kubwa zaidi. Amesema wamepata ushahidi kuwa Micah Johnson alifanya majaribio ya kulipuwa vilipuzi.

5. Waziri wa Misri aitahadharisha Israel

Image copyrightGETTY
Waziri wa mambo ya nje wa Misri , Sameh Shoukry, ameonya kuwa uwezekano wa kupatikana amani na usalama unafifia kwa Israeli ili mradi mzozo na raia wa Palestina unaendelea.
Aliyasema hayo katika ziara iliyo nadra nchini Israeli, inayotokea wakati Israel imeahidi takriban dola milioni 13 kwa ujenzi wa makazi ya walowezi katika ukingo wa magharibi.

6. Maafisa wa Israel kumchunguza Netanyahu

Image copyrightAP
Wizara ya haki Israeli inasema mkuu wa sheria nchini humo ameagiza uchunguzi dhidi ya inachokitaja kuwa masuala yanaomhusu waziri mkuu Benjamin Netanyahu. Imetoa taarifa kidogo lakini imesisistiza kuwa sio uchunguzi wa kihalifu. Msemaji wa waziri mkuu ameeleza kuwa uchunguzi huo hautobaini chochote.


SHARE

 • Image
 • Image
 • Image
 • Image
 • Image
  Blogger Comment
  Facebook Comment

1 comments:

 1. HIZI NDIO HABARI KUU ZILIZOGONGA VICHWA VYA HABARI DUNIANI LEO.. ZISOME HAPA ZOTE KUJUA MATUKIO MAKUBWA YA ELO DUNIANI.

  Miongoni mwa habari nyingine kuu leo, Umoja wa Mataifa umehimiza pande zote kusitisha vita Sudan Kusini, na Korea Kaskazini ikaitahadharisha Marekani

  ReplyDelete