CHADEMA YANYOOSHA MIKONO KWENDA DODOMA KUZUIA MKUTANO WA CCM 'MBOWE AWAOKOA MAKAMANDA VIJANA WA RED BRIGEDE CHADEMA KWENDA KUPAMBANA NA GREEN GUARD WA CCM DODOMA.'


MBOWE AWATAKA VIJANA WA CHADEMA KUTOKWENDA DODOMA MPAKA UTARATIBU MPYA UTAKAPOTOLEWA

Mwnyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe jana Jumapili 10/06/2016 amewataka vijana wa CHADEMA nchi nzima waliokuwa wamejiandaa kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kulisaidia jeshi la Polisi kuwaambia wanachama wa CCM kutii tamko lililotolewa na Rais Dkt. John Magufuli ya kufuta shughuli zote za siasa ikiwemo mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani, makongamano n.k kutokwenda tena Dodoma mpaka utaratibu mpya utakapotolewa.
Akiongea katika semina ya Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri wanaotokana na CHADEMA jijini Arusha leo, Mbowe ametumia fursa hiyo kulitaka Jeshi la polisi kuacha kupendelea Chama kimoja, na waelewe kwamba Rais ni mwanasiasa, amechaguliwa kupitia Chama cha siasa, shughuli anazozifanya ni za kisiasa, Waziri Mkuu,Wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya nao wanafanya shughuli za siasa.
"Nawataka vijana wote nchi nzima waliokuwa wanajiandaa kuelekea Dodoma, waache kwenda mpaka watakapojulishwa utaratibu mwingine kutoka ndani ya chama, kwa sababu Polisi wanapanga kufanya jambo ovu, kwani wameanza kuwakamata viongozi wa BAVICHA, waliokuwa wapo Dodoma, amekamatwa Patrobas Katambi ambaye ni Mwenyekiti wa BAVICHA na Julius Mwita ambae ni Katibu wa BAVICHA Taifa, wamekutwa wakila chakula wakakamatwa, kwa sababu Bwana Katambi ni Mwanasheria alitaka kujua kosa lake, lakini walimpiga, hili ni jeshi gani la Polisi lisilotambua wajibu, kulinda raia na mali zao" amesema Mhe. Mbowe.
Sheria ya vyama vya siasa na Marekebisho yake yote, yanatambua haki za vyama vya siasa kufanya shughuli zake za siasa bila kuvunja Sheria, huku Jeshi la Polisi likitoa ulinzi huo ukiwa ni wajibu wake.
Mbowe amesisitiza kwamba hawataomba tena kibali kwa jeshi la Polisi wala mamlaka yeyote, lakini wanabuni njia nyingine ya kufanya siasa, kwa sababu siasa ni maisha ya kila siku.
Wanakataza shughuli za kisiasa kwa sababu hawataki kukosolewa, wakati kuna mambo mengi sana ya kuikosoa Serikali, Serikali isiyotaka kukosolewa sio sikivu kwa wananchi inawaongoza.
Mhe. Mbowe amesisitiza kuwa wataendelea kupagania haki ya Taifa hili mpaka haki itakapotendeka, shauri lililokuwa limefunguliwa jijini Mwanza kupinga zuio la mikutano ya hadhara na maandamano jijini Mwanza, hivyo shauri hilo limehamkshiwa Mahakama Kuu Dar es salaam kupinga zuio la mikutano ya hadhara, maandamano, na shughuli mbalimbali, yakiwemo makongamano, mikutano ya ndani ya vyama vya siasa n.k.
Akiongea katika Semina ya Mameya na Wenyeviti wa halmashauri zinazotokana na CHADEMA, Mbowe amewataka wahakikishe wananchi waliowachagua wanawatumikia ipasavyo, kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana kwa wananchi, kama afya,elimu n.k, Mbowe amewataka viongozi hao wawe wabunifu zaidi katika kutatua matatizo ya Wananchi waonyoshe tofauti kwa sababu Wananchi wamewaamini.
"Kuna tatizo kubwa sana la ajira nchini, hakikisheni mnatengeneza fursa za kutosha ambazo zitawapa vijana na watu wote ajira, maisha yamekuwa magumu maradufu, kila kukicha bora ya jana, nyie kama viongozi wa maeneo yenu kaeni na wananchi wenu, mbuni fursa ambazo zitawafanya wananchi wenu waweze kujikwamua kiuchumi" Amesema.
Pia Mhe. Mbowe amewataka Viongozi hao kuacha kutoa pesa kwa vyama vya siasa, watu wa CCM kuwekewa mafuta na kupewa pesa kutoka Halmashauri, kuanzia sasa, Mhe. Mbowe amewataka viongozi hao kuwanyima, na wakiendelea atawaumbua, Halmashauri hazitakiwi kutoa pesa kwa vyama vya siasa, iwe CCM,CHADEMA, CUF n.k.
Katika semina hiyo ambayo imefungwa Rasmi na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe, pia umefanyika uchaguzi ambapo Meya wa jiji la Arusha,amechaguliwa kuwa Mwenyekiti,Katibu wake ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni,na Mnadhim amekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime.
Viongozi hao watatu,wamekuwa Wajumbe wa Kamati Kuu.
Imetolewa Na: Kurugenzi Ya Habari Chadema
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment