ZAIDI YA MILIONI 600 KUSHINDANIWA KUPITIA PROMOSHENI YA"KAMATA MPUNGA YA VODACOM"

•       Zawadi kubwa  ya promeshi ni kitita cha shilingi 100m/

•             Kutakuwepo na ushindi wa mamilioni kila siku,kila wiki na kila mwezi kati ya shilingi milioni 1 mpaka milioni 20

Vodacom Tanzania leo imezindua promosheni kubwa itakayowawezesha wateja wake kujishindia pesa taslimu kiasi cha shilingi Milioni 615 ndani ya siku 140.Promosheni hii inayojulikana kama ‘Kamata Mpunga’ ni mwendelezo wa moja ya malengo ya kampuni hiyo ya  kubadilisha maisha ya wateja wake kuwa bora.

Kampuni hiyo imekuwa ikiendesha promosheni mbalimbali za kubadilisha maisha ya wateja na watanzania kwa ujumla kama vile Mwaka jana iliendesha promosheni kubwa ambayo haijawahi kutokea nchini iliyojulikana kama Jaymillions ambayo ilibadilisha maisha ya wateja mbalimbali walioibuka washindi na maisha yao kuwa murua. Vilevile miaka ya nyuma kampuni iliwahi kuendesha promosheni kabambe kama vile timka na bodaboda na kampeni ya Mahela iliyomfanya Mwanafunzi wa Chuo cha elimu mkoani Kigoma kuibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 100/=.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema promosheni hii inajulikana kama ‘Kamata Mpunga’ inawahusisha wateja wote wa kampuni yetu na itawawezesha wateja watakaobahatika kushinda kuwa mamilionea, “kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku,kila wiki,kila mwezi na pia itakuwepo zawadi kubwa mwishoni mwa promosheni hii ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki.”

Nkurlu alisema kuwa kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kutakuwepo na washindi 3 wa shilingi Milioni 1/= kila mmoja na kila siku ya Jumapili atakuwepo mshindi wa Milioni 5/= na tarehe ya mwisho wa mwezi katika kipindi cha promosheni atakuwepo mshindi wa milioni 20/= na kuna mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ambaye atajinyakulia kitita cha Milioni 100/= ambazo zitatolewa katika kipindi cha mwisho cha promosheni.
Nkurlu amesema ushiriki wa promosheni hii utakuwa ni rahisi ambapo mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno “GO” kwenda namba 15544 ambapo atapata ujumbe wa kumfahamisha kuwa ameingia kwenye mchezo na ataanza kupokea maswali atakayotakiwa kuyajibu kwa ajili ya kujiongezea pointi za ushindi na mteja atakatwa shilingi  300 tu kwenye muda wake wa maongezi ”. Alisema.
Nkurlu alifafanua kuwa maswali atakayopokea mteja yatakuwa na majibu 2 moja likiwa jibu sahihi na lingine likiwa sio sahihi. Kila mteja  atakapokuwa  anajibu  atakuwa anafahamishwa iwapo amepata swali na ataweza kujipatia pointi. Aliongeza kuwa kila ujumbe utakaotumwa kwenda namba 15544 mshiriki atajipatia bonasi ya pointi 100 za kuanzia ambazo zitaongezeka kadri atakavyokuwa anajibu maswali.

Nkurlu alifafanua zaidi kuwa katika ushiriki wa kawaida kwenye promosheni hii mteja ataweza kujishindia pointi 20 kwa kila jibu la swali litakapokuwa sahihi na pointi 10 iwapo jibu lake sio sahihi. Pia kutakuwa na  bonasi  ambayo itatolewa kwa nusu saa hadi siku nzima kwa lengo la kuwawezesha wateja wengi kushiriki na kuwa na nafasi ya kujishindia zawadi ya mamilioni ya fedha. Alifafanua zaidi kuwa kutakuwa na nafasi ya  ushiriki kwa kujiunga moja kwa moja ambapo mteja atatakiwa kutuma neno “WIN” kwenda namba 15544 na atakakwa kiasi cha shilingi 200 tu. 

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salam leo(hawapo pichani)wakati wa Uzinduzi wa  Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno“GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali,Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa kampuni hiyo,Saurabh Jaiswal na Meneja wa huduma za ziada,Mathew Kampambe.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment