WAZIRI MWIGULU AFUNGA MAFUNZO YA POLISI CCP MOSHI

Hii leo waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Mwigulu Lameck MCHEMBA amefunga mafunzo ya jeshi la polisi-(Moshi Police Academy),wanafunzi 3904 wa jeshi la polisi na idara ya uhamiaji wamemaliza mafunzo yao.

Mbali na mambo mengine Mh Mwigulu awaonya Polisi na amesema "Kuna baadhi ya  watumishi wa jeshi la polisi wanakiuka miiko ya utumishi wao,tunapokea malalamiko ya watu kubabimbikiwa Kesi ,rushwa na kunyimwa haki mbalimbali. Natoa rai kwa watumishi wote wa jeshi la polisi , Msishughulike na wanyonge,shughulikieni kutatua matatizo ya wanyonge ili wajivunie kuwa na jeshi la polisi rafiki kwa raia wake."
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment