Uturuki yafungua ubalozi mpya Somalia

Image captionUbalozi wa Uturuki
Rais wa Uturuki amefungua ubalozi mpya katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Ijumaa huku kukiwa na usalama wa hali ya juu siku moja tu baada hoteli moja kushambuliwa na kupelekea vifo vya watu 15.
Kundi la wapiganaji la al-Shabab ambalo linakabiliana na serikali ya Somalia limekiri kutekeleza shambulo hilo katika hoteli ya Ambassador mjini Mogadishu.
Ziara hiyo ya rais Reccep Tayyip Erdogan ni ya tatu nchini Somalia.
Ni rais wa pekee anayetoka nje ya Afrika kutembelea taifa hilo lililokumbwa na vita kwa miongo kadhaa.
Erdogan alitembelea Somalia mwaka uliopita,siku moja baada ya al-Shabab kushambulia hoteli iliokuwa na wajumbe wa Uturuki na kuwaua takriban watu sita.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment