TANAPA YASAIDIA UJENZI WA MIUNDOMBINU KATIKA MAENEO YANAYOPAKANA NA HIFADHI YA TAIFA MILIMA YA MAHALE ILIYOPO MKOANI KIGOMA


Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima ya Mahale,Mhifadhi Romanus Mkonda akizungumza juu ya ujenzi wa madaraja ulioanza katika barabara ya kuelekea katika hifadhi hiyo.
Wanahabari wakimsilikiliza Mhandisi kutoka kampuni ya ujenzi ya Lilangela inayojenga daraja la Lagosa katika barabara ya Buhingu wilayani Uvinza ,Marango Ngose alipokuwa akizungumzia juu ya ujenzi huo unaofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kibao kinachoonesha taarifa mbalimbali juu ya ujenzi wa daraja hilo.
Baadhi ya mafundi wakijaribu kuchimba udongo katika eneo la mto Lagosa ambako daraja hilo linajengwa.
Baadhi ya malighafi zinazotumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo zikiwa eneo la ujenzi.
Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili kuta tatua changamoto ya wananchi katka vijiji hivyo kuvuka kwenda upande mwingine ambako kwa sasa wamekuwa wakilazimika kuvuka katikati ya mto huku wakiwa wamebeba vyombo vyao vya usafiri na hata mifugo imekua ikipita katika mto huo.
Ari kadharika kina mama na watoto kwa sasa wamekua wakilazimika kwenda kupata huduma ya maji upande wa pili wa mto huo na kwamba wanalazimika pia kupita ndani ya mto huo ili kuvuka kwenda katika makazi yao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwa ameongozana na wanahabari wakitoka katika eneo kunako jengwa daraja hilo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyeko Kigoma.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetoa Sh. Milioni 584 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ikiwa ni njia 

moja ya kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Milima ya Mahale vilivyopo wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma. 

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika vijiji vya Lukoma na Igalula wanakabiliwa na changamoto ya barabara jambo linalowafanya washindwe kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea vijiji hivyo vilivyoko mwambao mwa zimwa Tanganyika ,Mkuu wa idara ya ujirani mwema ,Mhifadhi Romanus Mkonda aliyataja madaraja hayo kuwa Lagosa na Lukoma.

“Daraja la Lagosa linatumia Sh. Milioni 296 wakati lile la Lukoma litatumia Sh. Milioni 288,” alisema.

Alisema lengo la TANAPA ni kusaidia jitihada za serikali za kuimarisha mawasiliano ya barabara katika ukanda huo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.

“Iwapo barabara hiyo itapitika itarahisisha usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa ukanda huu na pia Hifadhi yetu itaweza kupata watalii wengi kwa sababu usafiri uliopo sasa hivi ni wa maji na Ndege pekee,” alisema.

Hata hivyo, alisema iwapo miundombinu hiyo ya barabara itakamilika itaepusha gharama kubwa ambazo Hifadhi inaingia kwa ajili ya kwenda mjini kununua vitu mbalimbali vya hifadhini.

Aliongeza kuwa barabara hiyo itawasaidia wananchi hao kupata huduma mbalimbali zinazopatikana nje ya eneo lao ikiwa ni pamoja na kusafirisha mazao na kuyapeleka masoko ya nje.

“Kwa mfano tunapotaka kwenda mjini tunatumia Boti ambalo linatumia Lita 1000 za petroli kwenda na kurudi na oil lita 40...hivyo iwapo barabara zitakamilika gharama hizi zitapungua,” alisema.

Pia, alisema barabara hizo zikikamilika utalii utaongezeka na kuliongezea taifa pato.Aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/17, TANAPA imetenga Sh. Milioni 500 kwa ajili ya kujenga madaraja ya Nkonkwa na Igalula yaliyopo vijijini hapo.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Igalula, Mussa Matililo alisema iwapo madaraja hao yatakamilika itawarahisishia wananchi wa maeneo hayo katika shughuli zao za kilimo.

“Pia, itarahisisha mawasiliano ya kijiji kimoja kwenda kijiji kingine kwa sababu kwa sasa mawasiliano yamekuwa magumu kutokana nah ii mito miwili,” alisema.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment