TaGLA na TBA wakamilisha Mafunzo ya Siku Tano ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao

Wadau kutoka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) pamoja na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza mtoa mada kwa njia ya video (Tele Conference) wakati wa Mafunzo ya Siku Tano yaliyolengwa kwa ajili ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhusiana na masuala mbalimbali yanayaohusu majengo 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.

Meneja Mafunzo toka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Dickson Mwanyika akiwashukuru wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakati wa ufungaji jan 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mdau kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma akichangia mada kuhusiana na mafunzo ya siku tano waliyopatiwa na Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Elius Mwakalinga akitoa neno la sukurani kwa mtoa mada (hayupo pichani) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tano yaliyoaratibiwa na Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya siku tano kwa njia ya mtandao akipokea cheti chake toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Senkondo (katikati) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Elius Mwakalinga (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoaratibiwa na Ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo akiwashukuru wateja wake mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tano yaliyoaratibiwa na Ofisi yake 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment