SERIKALI YATAKIWA KUSHIRIKISHA SEKTA BINAFSI - SHEFFU

SERIKALI YATAKIWA KUSHIRIKISHA SEKTA BINAFSI - SHEFFU

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SERIKALI  imetakiwa kushirikisha sekta binafsi katika ujenzi wa miundombinu ili kuifanya sekta hiyo iweze kutanuka na kuongeza ajira nchini.

Akizungumza na  wadau wa biashara leo  katika hoteli ya Double Tree  wakati wa kujadili bajeti iliyowasilishwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Bungeni Mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Kampuni ya EY Tanzania,  Joseph Sheffu, amesema kuwa  kuweza sekta binafsi kuweza kutanuka serikali  inawajibu kushirikiana kwa baadhi ya miradi ikiwemo ujenzi wa barabara.

Amesema kuwa bajeti ni  nzuri kutokana na serikali kusimamia ulipaji wa kodi ambayo nchi zote zimeweza kusonga mbele kwa kuweka mbele kiumbele cha kodi.

Sheffu amesema kuwa, katika bajeti hii inahitaji kuwa na bajeti ya wafadhili ambayo inatakiwa kuwa na masharti nafuu , kuacha tusihitaji inaweza  kusababisha baadhi ya miradi kukwama.

Aidha  amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejitahidi kuja bajeti yenye unafuu kutokana na serikali imeingia ikiwa haina kitu lakini katika ukusanyaji wa mapato imejitahidi sana.

Sheffu amesema kuwa sasa serikali iweke kipaumbele cha kilimo kwani kumekuwepo na mkazo lakini matokeo katika sekta ya kilimo hayaonekani.
Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya EY Tanzania, Joseph Sheffu akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa kujadili bajeti kuu ya Serikali iliyowasilishwa jana Bunge na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango. Mkutano huo uliondaliwa na Kampuni ya Kimataifa ya Ernest Young (EY), umefanyika leo Juni 9, 2016 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree, Jijini Dar es salaam na kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.

Mmoja wa wachumi Nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Prof. Sufiani Bukurura akisisitiza jambo wakati akichangia mada katika Mkutano wa kujadili bajeti kuu ya Serikali iliyowasilishwa jana Bunge na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango. Mkutano huo uliondaliwa na Kampuni ya Kimataifa ya Ernest Young (EY), umefanyika leo Juni 9, 2016 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree, Jijini Dar es salaam.

Sehemu ya Wadau wakifatilia mbada mbali mbali kwenye Mkutano huo.

SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment