Mlipuko wakumba hoteli mjini Mogadishu

Image copyrightREUTERS
Image captionWanajeshi wa Amisson nchini Somalia
Mlipuko mkubwa umekumba hoteli moja katikati ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kuna sauti za ufyatulianaji wa risasi katika kile kinachoaminika huenda ni shambulio la wapiganaji wa al-Shabab.
Kulingana na mwandishi wa BBC Ibrahim Aden mjini Mogadishu, mlipuko huo ulikumba hoteli ya Naso Hablod ikiwa ni hatua chache kutoka kwa uwanja wa ndegewa mji huo.
Hakuna ripoti zozote za majeruhi.
Ripoti zinasema kuwa huenda kulikuwa na mlipuko wa pili.
Image copyrightREUTERS
Image captionShambulio Somalia
Wapiganaji wa al-Shabab hutekeleza mashambulio ya mara kwa mara katika mji huo kwa lengo la kuiangusha serikali inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.
''Walianza na mlipuaji wa kujitolea muhanga na baadaye kuvamia.Kwa sasa wako ndani na ufyatuliaji mkubwa wa risasi unaendelea'' ,alisema msemaji wa polisi meja Nur Farah.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment