MICHEZONI VIWANJANI..Euro2016 : Switzerland yailaza Albania

Image captionSwitzerland dhidi ya Albania
Switzerland imejipatia ushindi wake wa pili katika michuano ya bara Ulaya baada ya kuilaza Albania 1-0.
Mapema Albania ilionekana kubabaika pale mlinda lango wao Etrit Berisha alipofanya makosa kufuatia Krosi iliopigwa na Xherdan Shaqiri na hivyobasi kuwa rahisi kwa Schar kufunga kwa kichwa.
Lakini baadaye Armando Sadiku alikosa nafasi ya wazi kabla ya nahodha wa kikosi hicho Lorik Cana kupewa kadi ya manjano kwa kuunawa mpira.
Hatahivyo kushindwa kwa Switzerland kuongeza mabao kulifanya matokeo kusalia 1-0,lakini Shkelzen Gashi karibu asawazishe kwa upande wa Albania.
Mchezaji huo wa ziada alipata pasi nzuri huku ikiwa imesalia dakika tatu lakini Kipa Yann Sommer akaupangua mkwaju wake .
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment