MASHINDANO YA KUSOMA NA KUHIFADHI QUR'AN MBAGALA BUCHA JIJINI DAR ES SALAAM

 Na  Tamimu Adam
Wazazi na walezi wa kiislamu wametakiwa  kuenzi na kuihifadhi Quran  tukufu  na kuipa heshima ya aina yake kwa kuwahamasisha watoto wao kushiriki katika mashindano ya kusoma na kuifadhi Quran  ili kuwawezesha kufahamu vizuri uislamu na  kuwa muongozo katika maisha yao ya kila siku hapa dunia na kesho ahera.
 Hayo yalisemwa na Ustaadhi Iddrisa kutoka Kigoma  wakati wa mashindano ya kusoma na kuifadhi qurani yaliandaliwa na Madrasa  ya AL-Mustakima iliyopo mbagala  bucha jijini, Dar es salaam ambapo  watoto wa kiislamu takribani kumi (10) wenye umri kati ya miaka sa sita hadi kumi na tatu  wa madrasa  nne  ambavyo ni Madrasa  Tul – Mustakima  ya yombo dovya na mbagala bucha, madrassa Tul- ukutani  na madrassa Tul Ismailia ya mtoni kijichi. 
Naye  Mwalimu mkuu wa Madrasa ya AL- mustakima  ambayo ndio mratibu wa mashindano hayo Ustaadhi Hassani Suleimani  alisema  mashindano hayo yalishirikisha   wanafunzi kumi ambao waligawanywa katika makundi makuu mawili  kundi la kwanza ni wanafunzi watano kutoka vyuo vyote nne ambao walisoma na kuifadhi juzuu mbili na kundi la pili ni kwa wanafunzi ambao walisoma na kuifadhi juzuu tano.
Aidha ,  aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuwafundisha vijana kusoma na kuhifadhi kitabu cha mwenyezi mungu, kuipenda qurani na kuitumia katika maisha yao yote  pamoja na kuwafundisha maadili ya kiislamu  na maamurisho yake yote kwa waislamu. Aliongeza kuwa mashindano hayo yalisimamiwa na majaji watatu kutoka mbande ambao kwa ujumla walikuwa wanaangalia  vigezo mbalimbali ikiwemo namna ya kusoma na kutamka maneno ya quaran kwa usahihi.
Kwa upande wake  Imamu wa Msikiti wa mbagala charambe  Sheikh  Adam Mikidadi  ambaye alikuwa miongoni mwa majaji wa mashindano hayo alisema kuwa mashindano yalienda vizuri  ambapo yalifanyika kwa kiwango kilichotarajiwa,  washiriki walisoma na kutamka quarani vizuri kabisa na kuweza kufikia vigezo vya mashindano kwa asilimia 85.
Sheikh aliwataka washiriki wote kuongeza bidii mwakani ili waweze kufikia asilimia 100 na kuwa mahiri katika kusoma, kuhifadhi  na kukuza uislamu ndani ya jamii. 
Pia aliwataka wazazi na walezi kuhamasika  na kuisoma quaran tukufu ili iwe muongozo wao katika maisha yao yote na kwa wale wenye uwezo wawe na tabia ya kujitolewa kudhamini mashindano ya kusoma na kuhifadhi kitabu cha mwenye mungu.
Washiriki wa mashindano hayo walipewa zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza  Zahara Mohamed alizawadiwa shilingi laki moja na thelathini kwa kusoma na kuhifadhi juzuu 5 kati ya juzuu thelathini na wa pili  alizawadiwa fedha taslimu elfu themanini, tano na watatu alizawadiwa shilingi elfu sitini na tano na wengine walipewa elfu arobaini.

 Mwanafunzi wa Madrasa AL-Mustakima  Rashid Kimweli akisoma  Quaran katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quaran  yaliyofanyika  mbagala bucha, jijini Dar es salaam wakati wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran  yaliandaliwa na Madrasa  ya AL-Mustakima iliyopo Mbagala  Bucha jijini  Dar es salaam ambapo  watoto wa kiislamu takribani 10 wenye umri kati ya miaka  sita hadi 13   wa madrasa  nne  za Madrasa  Tul – Mustakima  ya Yombo Dovya, Mbagala Bucha, Madrassa Tul- ukutani  na madrassa Tul Ismailia ya mtoni kijichi. 

 Mwanafunzi wa madrasa  AL-Mustakima Zahra Mohamedi akipokea zawadi  shilingi laki moja na thelathini na tano ( 135,000) kwa kuibuka mshindi wa kwanza  wa kusoma na kuihifadhi juzuu tano kati ya thelathini  katika kitabu cha Quaran. 
 Mwalimu mkuu wa Madrasa AL- Mustakima  Ustaadhi  Hassani Seleiman akimtunza fedha ustaadh Iddrisa wakati wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran  yaliyoandaliwa na Madrasa AL mustakima ya Mbagala bucha jijini  Dar es salaam. 
Mwanafunzi wa madrasa  AL-Mustakima akipokea zawadi  shilingi laki moja na thelathini na tano ( 135,000) kwa kuibuka mshindi wa kwanza  wa kusoma na kuihifadhi juzuu tano kati ya thelathini  katika kitabu cha Quaran. ( Picha na Tamimu Adam).
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment