MANJI ASHINDA KWA KISHINDO, SANGA AMGARAGAZA OSORO HADI HURUMA

KAMA ilivyotarajiwa Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji (pichani) ametetea nafasi yake katika uchaguzi uliofanyika usiku katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Manji ambaye hakuwa na mpinzani, ameshinda kwa kukusanya zaidi ya asilimia 90 ya kura, huku Makamu wake, Clement Sanga akifanikiwa pia kutetea nafasi yake kwa kumshinda mpinzani pekee, Tito Osoro.

Sanga amekusanya zaidi ya asilimia 80 ya kura katika uchaguzi wa nafasi tatu, nyingine ikiwa ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amesema kwamba matokeo rasmi ya uchaguzi yatatangazwa leo.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment