'KAKA' KUIKOSA COPA AMERIKA CENTENARIO 2016, MESSI NAYE TIA MAJI TIA MAJI


Na Dac Popos, Globu ya Jamii.

Yakiwa yamesalia masaa machache kipyenga kupulizwa kuashiria ufunguzi wa michuano ya Copa Amerika, kiungo mahili na mkongwe wa timu ya taifa ya Brazil Ricardo Kaka ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo baada ya kuumia kifundo cha mguu. Kaka ambaye naye alichukuwa pahala pa kiungo wa Bayern Munich Douglas Costa, sasa na yeye nafasi yake itazibwa na kiungo kutoka klabu ya Sao Paulo, Henrique Gauso.
Kwa upande mwingine mchezaji bora wa Dunia mara tano, Lionel Messi aliwapa wakati mgumu mashabiki wake na waargentina kwa ujumla kuwa naye angekosa michuano hii kufuatia kupandishwa kizimbani katika mahakama moja nchini Hispania baada ya kushitakiwa kwa kosa la kukwepa kodi. 
Messi ameshitakiwa pamoja na Baba yake kwa kosa hilo, wote wawili wakana kosa hilo na Messi amesema yeye hafahamu chochote kinachoendelea kwa sababu kazi yake ni kucheza mpira tu na mambo yake mengine ya nje ya uwanja yanafanywa na watu wengine wakisimamiwa na Baba yake, Baada ya hapo Messi alipanda ndege kuelekea Marekani ili kujinga na wenzake kwa ajili ya mtanange huo wa michuano ya COPA AMERIKA CENTENARIO.

Kwa ufupi tena tuzidadavue timu mbili ambazo nchi zao zinadaiwa kwa kuwa na magenge makubwa ya wauza dawa ya kulevya (kwa lugha ya mtaani wanaita ngada), lakini sisi hayo hayatuhusu.
MEXICO

Kwenye viwango vya ubora wa soka vya shirikisho la soka duniani FIFA, mexico inakamata nafasi ya 16. Ikiwa kundi C na nchi za Jamaica, Uruguay na Venezuela, Mexico itawategemea sana nyota wake vijana kama vile mshambuliaji Javier Hernandez'chicharito' wa klabu ya Bayer Leverkeusen, mlinzi Paul Aquilar kutoka Club America, kiungo wa Porto Hector Herrera na Oribe Peralta wa Club America, chini ya kocha JUAN CARLOS OSRIO wanazungumziwa kuwa wataleta ushindani sana.
COLOMBIA

Chini ya kocha mzoefu JOSE PEKERMAN colombia ikiwa na wachezaji wanyumbulifu na vijana wengi ambao hutumia zaidi mchezo wa kumiliki mpira watatoa upinzani mkubwa katika kundi lake na hasa katika mechi ya ufunguzi kati yao na wenyeji Marekani.Ikiwa katika nafasi ya 4 ya ubora wa viwango vya FIFA, colombia itawategemea zaidi akina James Rodriguez wa Real Madrid, mshambulizi Roger Martinezwa Rancing Club, kiungo wa Juventus Juan coudrado na mshambulizi Carlos Barca wa As Milan.

Kipyenga kinapulizwa leo hivyo pitia kurasa hii ili upate kila kinachojiri huko Marekani
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment