CHADEMA YAPANGA SAFU YA KIKOSI KAZI 'KUIONDOA' CCM 2020. JE UNAIJUA SAFU HIYO INGIA NDANI UJUE WALIOTEULIWA...


SAFU MPYA WATUMISHI CHADEMA.
Waheshimiwa,
Nawasalimu: CHADEMA - VEMA.
Naomba niwataarifu maendeleo ya REFORMS katika secretariat na Kanda wakati mkisubiri waraka wa KM ambao utatoa hadidu za rejea katika kipindi kilicho mbele yetu kuelekea uchaguzi mkuu 2020. Nimejikita zaidi katika maendeleo ya uteuzi katika kujaza nafasi muhimu za watendaji ndani ya chama.
Kama mjuavyo, kutakuwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama, ambaye ni Mh. Tundu A. M. Lissu.
Baada ya kutafakari kwa kina, wafuatao watachukua nafasi zilizo kwenye mabano:
Mh. Meshack Micus Michael (Katibu - Victoria)
Mh. General Kaduma (Katibu - Magharibi)
Mh. Amani Golugwa (Katibu - Kaskazini)
Mh. Filbert Ngatunga (Katibu - Kusini)
Mh. Frank Mwaisumbe (Katibu - Nyasa)
Mh. Casmir Mabina (Katibu - Pwani)
Mh. Idd Salehe Kizota (Katibu - Kati)
Mh. Renatus Nzemo (Katibu - Serengeti)
Pia kutakuwa na wakurugenzi 5 na mpaka sasa nafasi tatu zimejazwa na mbili bado zinafanyiwa kazi:
Mh. John Edward Mrema (Mkurugenzi - Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya nje)
Mh. Benson Singo Kigaila (Mkurugenzi - Ulinzi na Usalama)
Mh. Roderick Lutembeka (Mkurugenzi - Fedha, Uchumi na Utawala)
TBD (Mkurugenzi - Sheria na Haki za Binadamu)
TBD (Mkurugenzi - Bunge na Halmashauri)
Katiba muundo huu, pia kutakuwa na maafisa 4 wataalamu ndani ya ofisi ya KM ambao watakuwa wajumbe wa secretariat:
Mh. Reginald Munisi (Mkuu wa Kitengo - Oganaizesheni na Uchaguzi)
Mh. Robert Renatus Bujiku (Mkuu wa Kitengo - Ufuatiliaji na Tathmini)
TBD (Tehama)
TBD (Mkaguzi wa Ndani)
Kwa taarifa hii fupi, wale wote ambao majina yao hayajatokea hapa; watapangiwa kazi nyingine kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa.
Naomba kwa sasa Waratibu Kanda wote mwendelee kushikiria nafasi zenu mpaka pale mtakapo kabidhi kwa Makatibu wa Kanda. Natarajia Waratibu-Kanda wote watawahabarisha viongozi wa kisiasa katika maeneo yao.
Ningependa sana makabidhiano haya yawe yamekamilika ifikapo Juni 30, 2016.
Niwatakie kazi njema.
Pamoja na salaam za chama.
Dr. Vincent B. Mashinji
Secretary General
Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment