BRAZIL YASHIKA KASI COPA AMERIKA, YAITANDIKA HAITI BAO 7-1, PERU NA EQUADOR ZAVUTANA SHATI


Na Dac Popos, Globu ya Jamii. 
Katika muendelezo wa Michuano ya Copa Amerika, alfajini ya leo kumepigwa mechi mbili katika za kundi B ikiwa ni Brazili vs Haiti na nyingine ni Peru vs Equador.

Phillipe Coutinho alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 3 (hart trick)katika michuano ya Copa America inayoendelea kutimua vumbi nchini Marekani, mchezo huo uliopigwa usiku mwingi wa kuamkia leo,Coutinho ndiye aliefungua kalamu hiyo ya mabao kunako dakika ya 13 kwa shuti la kukunja la umbali wa mita20 na kuongeza goli lingine jepesi dakika ya 28. Kunako dakika ya 34 Renarto Augusto akaipatia Brazil goli la 3,na hadi mapumziko Brazil 3, Haiti 0.

Iliwachukuwa tena Brazil dakika 13 toka kuanza kipindi cha pili ikimaanisha dakika ya 58 pale Gabriel alipofunga bao la 4.Kama hiyo haitoshi Lucas Lima akafunga bao la 5 dakika ya 66 lakini dakika 3 baadaye Haiti wakajipatia goli la kufutia machozi kupitia kwa nyota wake James Marcell.Dakika ya 85 Renarto Augusto akafunga bao la 6 huku Phillipe Coutinho akihitimisha kalamu hiyo ya mabao katika dakika ya 90 na kufanya mambano kwisha jumla ya mabao 7-1.
Katika mchezo mwingine uliokuwa wa kusisimua Peru na Equador ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.Peru iliongoza kwa mabao 2-0 kwa muda mrefu wa kipindi cha kwanza kwa magoli yaliofungwa na Christian Cueva dakika 5 ya mchezo na Edison Flores kwenye dakika ya13. Nayo Equador ilisawazisha kupitia kwa wachezaji Enner Valenciadakika ya 43 na Miller Balanos kunako dakika ya 47.

Leo usiku mwingi wa kuamkia kesho ni vita kati ya

PARAGUAY vs VENEZUELA
na
MEXICO vs JAMAICA
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment