Aliyewahi kuwa Makamo wa rais wa Congo DRC Jean Pierre Bemba kushtakiwa

Image copyrightGETTY
Image captionJean Pierre Bemba
Jean Pierre Bemba,mwanasiasa wa zamani nchini Congo, amekutwa na hatia na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita dhidi ya binaadamu, na uhalifu wa kivita, na anatarajiwa kuhukumiwa hii leo.
Mahakama hiyo iligundua kuwa majeshi yake yaliyokuwa yakijulikana kama Congolese liberation army, aliyaelekeza kueneza mashambulizi dhidi ya raia katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ,kati ya mwaka 2002 na mwezi March mwaka 2003.
Mwendesha mashitaka amemhukumu Bemba kifungo cha miaka 25 jela . Mwandishi wa BBC Maud Jullien ana taarifu zaidi.
Jean Pierre Bemba,amekutwa na hatia ya kushindwa kuyadhibiti majeshi yake kuacha kuua na ubakaji raia ndani ya Jamhuri ya Africa ya Kati, mahali ambako inadaiwa alipeleka zaidi ya wapiganaji 1000 kuzuia kikundi cha uasi.
Image copyright
Mashtaka ya ubakaji yameibuliwa kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo kimataifa ya uhalifu, hatua ambayo imepongezwa na makundi ya haki za binadamu.
Mwanasheria wa Bemba tayari amekwisha toa msimamo wa upande wao kwamba watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mahali alipowahi kuwa makamu wa kwanza wa rais, Bemba bado anaendelea kufurahia uungwaji mkono kutoka kwa wanachama wa chama chake MLC, ambao wengi wao wanaamini kwamba ataachiliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa rais ambao umepangwa kufanyika mwezi November.
ambao wengi wao alitegemea itakuwa iliyotolewa katika muda kwa ajili uchaguzi wa rais ambayo imepangwa kufanyika mwezi Novemba.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment