Wema Sepetu Achukua Pointi Tatu Kwa Kumuombea Kura za BET Awards Diamond

Inaonekana somo la uzalendo limewaingia vyema mastaa wetu licha ya tofauti zao. Baada ya hivi karibuni Alikiba kuwaomba watanzania wampigie kura Diamond anayewania tuzo za BET, Wema Sepetu naye amefanya hivyo.

Wema ametumia Instagram kuwaambia mashabiki wake wampigie kura ex wake huyo aliyetajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa.

“Uzalendo ndo unaotakiwa… Tanzania Kwanza Vingine Baadae… Ama nene…? Vote Vote Vote….,” ameandika Wema kwenye picha ya BET Awards aliyoiweka Instagram.

Mashabiki wengi wamempongeza kwa uzalendo huo aliounesha licha ya yeye na Diamond kuwa mbali kwa sasa kutokana na kila mmoja kuwa na maisha yake. Wema na mpenzi wa sasa wa Diamond ni paka na panya.

Diamond anachuana na mastaa wengine wa Afrika wakiwemo Wizkid, Yemi Alade, AKA, Cassper Nyovest na wengine wawili.

Hii ni mara ya pili kwa muimbaji huyo wa Make Me Sing kutajwa kuwania tuzo hizo kubwa duniani.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment