Watu Saba wapatwa na hatia mashambulio ya Mabomu Kampala

Kifo

Image captionWaliopatikana na hatia wanakabiliwa na hatari ya kuhukumiwa ya kifo
Watu saba kati ya 13 waliokuwa wameshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu ya mwaka 2010 mjini Kampala wamepatikana na hatia.
Mashambulio hayo, yaliyotekelezwa katika maeneo mawili watu walipokuwa wakitazama fainali ya Kombe la Dunia, yalisababisha vifo vya watu 74.
Jaji Alfonse Owiny-Dollo ameamua watu sita kati ya walioshtakiwa hawakuwa na hatia.
Jaji, akitegemea sana ushahidi wa watu wawili waliokiri kuhusika na kuhukumiwa, alisema Isa Ahmed Luyima ndiye aliyehusika sana katika mashambulio hayo.
Kundi la al-Shabab kutoka Somalia lilidai kuhusika.
Jaji awali aliwaondolewa mashtaka ya kuwa wanachama wa kundi la kigaidi akisema kundi la al-Shabab wakati huo halikuwa limeorodheshwa kuwa kundi la kigaidi nchini Uganda.
Luyima
Image captionJaji amesema Isa Luyima alikuwa mhusika mkuu
Waliopatikana na hatia ni: Isa Ahmed Luyima, Hassan Haruna Luyim, Habib Suleiman Njoroge, Suleiman Hajjir Nyamandondo, Idris Magondu, Hassan Hussein Agade na Muhammed Ali Muhammed.
Walioondolewa mashtaka ni Omar Awadh Omar, Muzafar Luyima, Abubakari Batemyeto, Yahya Suleiman Mbuthia, Muhammed Hamid Suleiman na Dkt Kalule Suleiman.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment