WABUNGE SABA WAFUNGIWA KUHUDHULIA VIKAO VYA BUNGE


Wabunge, Tundu Lissu na Esther Bulaya wamefungiwa kuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya bunge la bajeti na bunge lijalo la mwezi wa tisa.

Vilevile Zitto Kabwe, Pauline Gekul, Godbless Lema na Halima Mdee wamefungiwa kushiriki vikao vilivyobaki vya bajeti na John Heche afungiwa kuhudhuria vikao kumi mfululizo vya Bunge la bajeti kuanzia leo.

Huu ni uamuzi wa Kamati  ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge chini Mwenyekiti George Mkuchika (Mb).

Wamekutwa na makosa mengi ya kukosa nidhamu na kutoheshimu Kiti Bungeni.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment