RC DAR, MGENI RASMI MAADHIMISHO YA HEDHI SALAMA


Mratibu wa Maji, Afya na Usafiri wa Mazingira kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Theresia Kuiwite (kulia). akizungumza  na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama. Wengine ni Mkurugenzi wa Programu za Afya Mashuleni kutoka Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Orsolina Tolage (kushoto) na Msemaji mwakilishi wa Wadau wote wa Mapendeleo waliochangia maadhimisho hayo, Clare Haule.
 Mkurugenzi wa Programu za Afya Mashuleni kutoka Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Orsolina Tolage (katikati), akizungumza  na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama. Kulia ni Msemaji mwakilishi wa Wadau wote wa Mapendeleo waliochangia maadhimisho hayo, Clare Haule na Mratibu wa Maji, Afya na Usafiri wa Mazingira kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Theresia Kuiwite.
 Msemaji mwakilishi wa Wadau wote wa Mapendeleo waliochangia maadhimisho hayo, Clare Haule  akizungumza  na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama. Kushoto ni Mkurugenzi wa Programu za Afya Mashuleni kutoka Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Orsolina Tolage (katikati).

Na Mwandishi wetu.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Hedhi Salama Duniani ambayo hufanyika   Mei 28 kila mwaka.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Kinga , Orsolina Tolage amesema kuwa suala hedhi salama wanaliangalia sana katika kuweza mazingira bora ya afya ya wasichana.

Amesema kuwa Wizara ya Afya Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejipanga kwa kushirikiana na wizara ya elimu na Sayansi na Teknolojia juu ya kuangalia watoto wa kike mashuleni wasiweze kukosa kusoma kutokana vifaa vya kumkinga katika hedhi.

Nae Mratibu wa Maji , Afya na Usafi wa Mazingira Mashuleni wa izara ya elimu na Sayansi na TeknolojiaTheresia Kiuwela amesema kuwa wasichana wanakosa masomo kwa miezi miwili kutokana na hedhi hivyo ni lazima siku hizo zisipotee kwa msichana kukosa kusoma.

Amesema kuwa wameweka utaratibu wa kupata tauro za kike (Ped) kwa sh.1000 ambapo baadhi ya wasichana hasa katika maeneo ya vijijini wanashindwa kukumdu gharama hizo.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment