Pwani za Libya kudhibitiwa sasa kulindwa kijeshi

Image copyrightBBC WORLD SERVICE
Image captionWaziri wa mambo ya nje wa Uingereza, William Hague, akitoa hotuba yenye ujumbe kuulinda mustakabali wetu.
Uingereza imetoa msimamo wake kwamba itapeleka meli na askari wa majini kutoka katika ufalme wake nchini Libya ili kusaidia kutoa mafunzo kwa walinzi wa pwani wawe na uwezo wa kuzuia biashara ya ulanguzi kwa watu wanaotaka kuvuka bahari ya Mediterranean.
Maofisa hao wameeleza pia kuwa wanatafuta kibali cha umoja wa mataifa kwa ajili ya meli ya kuzuia boti za magendo ya silaha dhidi ya kundi Islamic State.
Mapema, wahamiaji kadhaa wa kadhaa walihofiwa kuzama wakati mashua zao zilizo kuwa na msongamano mkubwa zilipopinduka pwani ya Libya.
Walinzi wa pwani ya Italia wanasema kwamba hatua hiyo imesaidia kuokoa maisha ya wahamiaji elfu nne waliokuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean wiki hii .
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment