MWANA UME MMOJA ANG'ATWA NA NYOKA KWENYE UUME WAKE WAKATI AKIJISAIDIA HUKO THAILAND

Attaporn Boonmakchuay

Image captionAttaporn Boonmakchuay
Raia mmoja wa Thailand anaendelea kuuuguza jeraha katika hospitali moja baada ya nyoka aina ya chatu kutokea ndani ya choo na kumng'ata uume wake.
Attaporn Boonmakchuay,ambaye alipoteza damu nyingi amesema kuwa nyoka hiyo ilikuwa ikimvuta baada ya yeye na mkewe kujaribu kuipiga.
Madaktari wanasema kuwa Bw Attaporn ambaye alipoteza damu nyingi anaendelea vyema na matibabu.
Image copyrightAP BBTV CH7
Image captionNyoka akitolewa katika choo hicho
Wafanyikazi walilazimka kukiharibu choo hicho.Baadaye nyoka huyo aliachiliwa na kuingia msituni.
Kisa hucho kilitokea wakati ambapo Attaporn mwenye umri wa miaka 38 alielekea katika choo chake nyumbani kwake huko Chachoengsao,mashariki mwa Bangkok kabla ya kwenda kazini siku ya Jumatano.
Wakati alipokuwa akitumia choo hicho alihisi uchungu mkali.
Image copyrightAPBBTV CH7
Image captionNyoka aina ya chatu
''Nilihisi kama ambaye uume wangu ulikuwa umekatwa,Nyoka huyo alikuwa akinivuta kwa kutumia nguvu nyingi'',alisema.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment