Mambo 3 Ambayo Inabidi Kila Mwenye Simu ya Android Ayafahamu


Ni sawa kabisa kuwa vifaa vya Android huwa vinakuja na mambo mengi mazuri ndani yake. Ukiachana na vipengele vya kawaida ambavyo karibia kila mtu mwenye simu ya Android anavijua kuna vile ambavyo kidogo havijulikani kwa kiasi kikubwa…usijali leo tutakuonyesha vitu 3 muhimu sana kufahamu!

Kufahamu mambo haya itakusaidia kuweza kutumia kifaa chako kwa ufanisi zaidi, kulinda usalama wa data zako bila ya kusahau kuwa na utumizi mzuri wa betri la kifaa chako cha Android


android animation
1> Punguza manjonjo ya Animation – Okoa chaji na ufanisi wa simu
Sawa wengine wanaweza kataa kufanya hivyo kwani wanaona kama vifaa vyao vinapoteza muonekano wake mzuri. Sawa ni kitu kizuri kuwa nacho lakini kwa kiasi kikubwa kinashusha ufanisi wa kifaa chako katika kufanya kazi yake kama inavyotakiwa.

Ili kupunguza Animation nenda katika Settings >> Developer Options >> Window animation Scale. hapo unaweza ukawa umepoteza ule mwonekano wako mzuri lakini nakuhakikishia kwamba utakuwa umeoneza kiasi cha ufanisi na hii ni kujumuisha na spidi katika simu yako .
Unaweza ukapunguza kiwango cha Animation mpaka 0.5X au unaweza amua kuizima kabisa ingawa ni vizuri zaidi kuipunguza tuu.


2> Desktop Backup Password – Zuia kuibiwa data kwa USB
Kila mmoja wetu ana tarifa zake za muhimu kama vile zile za kibenki, picha zile ambazo ni siri yako na mengine mengi ya siri katika simu yako. Na pia kumbuka hatutaka mtu aweze kuchukua Data za kwenye simu hii kwa kuunganisha na waya wa USB kwenye kompyuta.

Ili kuzuia aina hii ya wizi Android wana kipengele mahususi ambacho kinaweza kukusaidia katika hili. Unaweza weka nenosiri (password) kwa ajili ya ulinzi. Ulinzi huu utakuwa pale unapochomeka USB ili kuweza kuona mafaili yaliyopo katika kifaa kwa kutumia kompyuta basi itakulazimu uingize Nenosiri (password).
Ili kuliwezesha hili nenda katika Settings >> Developer Options >> Desktop Backup Password .Katika kifaa chako cha Android  Kitu kingine katika vifaa vyetu vya Android ni Background Data


3> Zuia Baadhi Ya Taarifa Nyuma Ya Pazia – Utumiaji wa data (intaneti)
Wengi wetu tunalalamika sana kuwa simu zetu hazikai na chaji na MB/GB zinaisha kimazingara. Ubaya wa chaji ya simu na hata bando ni kwamba huwa zinalika hata kwa zile App ambazo hatuzitumii muda huo ambazo zinajiendesha kwa siri nyuma ya pazia.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment